Rais Samia ateua bosi jeshi la polisi

Kamishna wa Polisi, Suzan Kaganda
Muktasari:
Suzan Kaganda anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi (CP), Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Oktoba 24, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Zuhura Yunus imeeleza Amri Jeshi Mkuu huyo wa vikosi vya ulinzi na usalama pia, amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Raslimali watu wa Jeshi la Polisi.
“Vile vile, Rais Sarnia amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Raslimali watu wa Jeshi la Polisi,” imesema taarifa hiyo.
Kamishna Kaganda anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi (CP), Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.