Rais Samia awaapisha mawaziri

Saturday April 02 2022
By Peter Elias

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewaapisha mawaziri watatu aliowabadilisha wizara hivi karibuni katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri aliyoyafanya Machi 31, 2022.

Mawaziri hao wameapishwa leo Aprili 2, 2022 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma sambamba na viongozi wengine walioteuliwa.

Mawaziri walioapishwa ni pamoja na George Simbachawene ambaye alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ameapishwa kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) wakati Pindi Chana aliyekuwa katika wizara hiyo ameapishwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

Dk Damas Ndumbaro aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, ameapishwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria akichukua nafasi ya Simbachawene.

Viongozi wengine walioapishwa ni pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Maadili, Ibrahim Mipawa pamoja na wajumbe wa baraza hilo.

Advertisement