Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rufaa ya Ma DED kutosimamia uchaguzi yaiva, majaji watano kuisikiliza

Muktasari:

Rufaa ya Serikali ya Tanzania kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwabatilisha kifungu cha sheria ya uchaguzi kinachowapa mamlaka wakurugenzi wa halmashauri za majiji, miji, Manispaa kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaghuzi (Nec) Julai 30, 2019.

Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani ya Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya Serikali ya Tanzania kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuwaengua wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa miji/wilaya  katika usimamizi wa uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika hukumu hiyo iliyosomwa na kiongozi wa jopo hilo la majaji waliosikiliza kesi , Dk Ngwala, mahakama hiyo ilisema kuwa kifungu hicho kinakinzana na matakwa ya Katiba ya Nchi inayotaka Tume ya Uchaguzi iwe huru.

 

Pia Mahakama hiyo ilibatilisha kifungu cha 7(3)  kinachoipa NEC mamlaka ya kumteua mtu yeyote miongoni mwa watumishi wa umma kuwa msimamizi wa uchaguzi, ikisema kuwa hakijabainisha namna gani kinatoa ulinzi kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yake kwa uhuru.

Hata hivyo, Serikali kupitia kwa Wakili wa Serikali Mkuu, ilikata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga sehemu ya hukumu hiyo hasa uamuzi wa kubatilisha vifungu hivyo.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya Mahakama ya Rufani vya Julai, 2019 rufaa hiyo imepangwa kusilizwa Julai 30, 2019 na jopo la Majaji watano.

Jopo la majaji hao linaongozwa na Jaji Augustine Mwarija akishirikiana na Jaji Stella Mugasha, Jaji Richard Mziray, Jaji Rehema Mkuye na Jaji Jacobs Mwambegele.

 

Hukumu hiyo  ya Mahakama Kuu ilitoka na kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na watetezi na wanaharakati wa haki za binadamu na demokrasia kwa kushirikiana na vyama vya siasa, wakiwakilishwa na mwanachama wa Chama Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bob Wangwe