Sabaya apona afika mahakamani, shahidi wa saba kuendelea kutoa ushahidi

Sabaya apona afika mahakamani, shahidi wa saba kuendelea kutoa ushahidi

Muktasari:

  •  Shahidi wa saba wa jamhuri, ASP Gwakisa Minga anaendelea kutoa ushahidi wake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo(Sabaya), kufika mahakamani.


Arusha. Shahidi wa saba wa Jamhuri, ASP Gwakisa Minga anaendelea kutoa ushahidi wake katika kesi ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya mshitakiwa wa kwanza katika shauri hilo(Sabaya), kufika mahakamani.

Minga ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Wilaya ya Arusha alianza kuongozwa juzi na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula.

Jana kesi hiyo ilishindwa kuendelea kusikilizwa kufuatia mshitakiwa huyo kushindwa kufika mahakamani kutokana na kuumwa.

Leo Alhamisi Agosti 5, 2021 Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo, Sabaya na wenzake wawili Sylvester Nyegu na Daniel Mbura waliwasili mahakamani hapo majira ya saa tatu asubuhi kwa ajili ya kuendelea na shauri hilo lililoanza kusikilizwa mfululizo kuanzia Septemba 19, 2021.

Mshitikiwa huyo alipoulizwa na hakimu huyo kuhusu maendeleo ya afya yake aliieleza mahakama kuwa anaendelea vizuri na anaweza kufuatilia mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ya jinai namba 105, 2021.