Samia: Serikali inakamilisha vigezo Chato kuwa Mkoa

Samia: Serikali inakamilisha vigezo Chato kuwa Mkoa

Muktasari:

  •  Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakamilisha vigezo vitakavyoruhusu Chato kuwa Mkoa.


Chato. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inakamilisha vigezo vitakavyoruhusu Chato kuwa Mkoa.

Akihutubia kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2021, leo Alhamisi Oktoba 14, 2021 Samia amesema iwapo vigezo vyote  vitakamilika Serikali itatangaza kuanzishwa kwa mkoa huo.

"Bado (Chato) haijawa Mkoa.....kuna vigezo kadhaa bado tunaviangalia na vigezo hivi vikikidhi basi tunakwenda kulimaliza jambo hilo”amesema.

Mchakato wa kuanzishwa kwa mkoa huo tayari umeanza kwa kujadiliwa na kupitishwa kwenye vikao vya ngazi ya wilaya na mkoa wa Geita.

Katika hotuba yake, Rais Samia pia amewahidi kuendeleza na kukamilisha miradi yote iliyanzishwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli ambaye ni mzaliwa wa Chato.

Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa bandari ya Nyamirembe, Uwanja wa ndege, Hospitali ya rufaa ya kanda, chuo cha ufundi stadii (Veta) na msikiti.