Serikali yaeleza faida za urasimishaji ardhi
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
Muktasari:
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema hayo alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Salma Mwassa aliyetaka kujua umuhimu wa kurasimisha ardhi maeneo ambayo hayajapimwa.
Dodoma. Mipango hiyo, kwa mujibu wa Serikali inapaswa kwenda sambamba na uimarishaji wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji wa mandhari ya nchi.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema hayo alipojibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Salma Mwassa aliyetaka kujua umuhimu wa kurasimisha ardhi maeneo ambayo hayajapimwa.
Mabula amesema urasimishaji huo maana yake ni kutambua miliki za wananchi kwenye maeneo yaliyoendelezwa bila kupimwa kisheria.
“Urasimishaji ni kazi shirikishi inayowezesha wananchi kukubaliana mipaka ya viwanja, kufungua njia na kutoa maeneo ya huduma za jamii kama vile shule, vituo vidogo vya polisi, makaburi, zahanati na maeneo ya wazi,” amesema.