Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yaombwa kuchunguza ukiukaji haki za wanahabari

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imeombwa kuchunguza ripoti zote za ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya waandishi wa habari na kuhakikisha wale wote waliotekeleza vitendo hivyo wanachukuliwa hatua.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imeombwa kuchunguza ripoti zote za ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya waandishi wa habari na kuhakikisha wale wote waliotekeleza vitendo hivyo wanachukuliwa hatua.

Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Program wa Shirika linaloshughulika na masuala ya kufanya utafiti kuhusu uhuru na haki za wanahabari la Article 19 kutoka Kenya, Sarah Wesonga wakati wa semina ya siku moja waliyoiandaa.

Pamoja Article 19 washiriki wengine wa uandaaji wa semina hiyo ni  Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Congress of Africa Journalist (CAJ) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

Wesonga amesema kwa mujibu wa ripoti yao ya utafiti walioufanya walibaini kuwa jumla ya waandishi wa habari watano Tanzania katika kipindi cha mwaka jana wakati wa ugonjwa wa Uviko 19 walifanyiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Kutokana na vitendo hivyo tunaiomba Serikali ya Tanzania kuchunguza ripoti zote za ukiukwaji wa wanahabari hao na kuwachukulia hatua za kisheria kulingana na viwango vya kimataifa wale wote watakaobainika kuhusika,” amesema.

Hata hivyo amesema kuwalinda waandishi wa habari, watetezi wa haki za binadamu na kutotii sheria kwa mashambulio dhidi yao ni suala linalopewa kipaumbele duniani kwa lengo la kulinda uhuru wa kujieleza.