Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serikali yawatoa hofu wananchi uhaba wa chakula

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika Jubilee ya miaka 50 ya tangu kuanzishwa Umoja wa Wanawake Wakatoliki Tanzania (Wawata) katika Sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo Jumapili Septemba 11, 2022.

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan awatoa hofu watanzania kuhusu usalama wa chakula akisema akiba iliyopo kwenye hifadhi ya ghala la chakula inatosheleza mahitaji ya taifa licha ya mavuno kuwa hafifu kwa msimu uliopita.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia Watanzania kuwa nchi ipo kwenye hali nzuri ya chakula licha ya mavuno hafifu yaliyopatikana msimu uliopita.

Amesema hayo wakati akitoa hotuba yake leo Septemba 11, 2022 kwenye sherehe ya kuhadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Wanawake wa Kanisa Katoliki Tanzania (Wawata) zilizofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Amesema “Tanzania bado tupo kwenye hali nzuri ya chakula licha ya mavuno hafifu kwa msimu uliopita. Kwenye ghala la taifa la kuhifadhi chakula tuna zaidi ya tani 150,000 tulizoziweka kwa ajili ya wakati mgumu.

Mwaka 2019/2020 ghala letu lilikuwa na tani 50,000 ambazo tulipoingia kwenye wakati mgumu ziliweza kusaidia watanzania na kupata zile za kusaidia nchi jirani sasa hivi tumeongeza uwezo wa ghala mara tatu ya iliyokuwa nyuma,”amesema

Amesema shabaha na imani ya Serikali kwamba akiba hiyo inalitosheleza taifa bila kuingia kwenye janga la uhaba wa chakula huku akiwataka watanzania kuendelea kumuomba Mungu ashushe mvua zenye neema.

Amesema Serikali imechukua hatua ya kutoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo ili kutoa hamasa kwa wakulima kwa kuwapunguzia gharama kubwa ya kununua pembejeo na mbolea kwa bei nzuri.

Awali Mwenyekiti wa Wawata taifa, Evaline Ntenga aliomba Serikali kuweka mipango madhubuti kuhakikisha watanzania hawakabiliwi na janga la njaa kutokana na kusuasua kwa mvua za msimu hali iliyochangia kupatikana mavuno kidogo.