Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh21 milioni zatengeneza gari la Zimamoto Shinyanga

Muktasari:

Gari hilo limerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kampuni ya Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Ltd kulifanyia matengenezo.

Shinyanga. Hatimaye changamoto ya ukosefu wa gari la zima moto na uokoaji limetatuliwa baada ya gari hilo kufanyiwa matengenezo na Mgodi wa Almasi wa Williamson Diamond Ltd uliopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani hapa kwa gharama ya Sh21 milioni.

Meneja Uhusiano Kampuni ya Williason Diamonds Limited, Bernard Mihayo akikabidhi gari hilo leo  kwa Kamanda wa Mkoa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Shinyanga, amesema  litasaidia uokoaji kwa wakati kwa sababu limewekewa vifaa vyote vilivyohitajika.

Mihayo amesema Kamanda wa Mkoa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, George Murutu baada ya kupeleka ombi la kutengeneza gari hilo kampuni ilikubali na kuanza matengenezo tarehe moja mwezi wa sita.

Amesema Septemba mosi walimaza matengenezo na Septemba 13 walikabidhi gari hilo tayari kwa uendelea na kazi ya uokoaji wa matukio ya moto Manispaa ya Shinyanga.

"Baada ya kukubali maombi ya Kamanda wa Zimamoto tulitenga muda wa kutengeneza gari hili huku tukiendelea na uzalishaji wetu wa almasi, kwa sababu na sisi ni sehemu ya jamii," amesema Mihayo.

Naye Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Shagembe Mipawa amesema kampuni hiyo inashirikiana vizuri na serikali kwa jambo lolote litakalotokea kwenye jamii.

Kwa upande wake, Kamanda Murutu amesema anaishukuru kampuni hiyo kwa kukubali ombi lao na kufanya matengenezo kwa wakati baada ya gari hilo kupata ajali ya barabarani na kupinduka likiwa katika majaribio ya barabarani baada ya matengenezo ya Injini kukamilika.

"Baada ya gari hili kupata ajali tulipata changamoto ya gari lakini tuliitika wito katika kuyakabili matukio ya moto na uokoaji kwa kutumia gari aina ya Isuzu ELF Pumper na ushirikiano wa magari makubwa ya Zimamoto kutoka kambi ya Jeshi ya Kizumbi, Kampuni ya Gaki Investment na Kiwanda cha Jambo Group yametusaidia sana," amesema Murutu.

Joseph George ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Shinyanga ameishukuru kampuni hiyo kwa kutoa msaada wa matengenezo ya gari kwa sababu magari ya kuomba yalikuwa yanachelewa kwenye matukio na kukuta kila kitu kimeshateketea.

Naye Mariam Paul ameishukuru Kampuni ya Williamson Diamond, akisema kwa matengenezo hayo gari litafika kwa wakati na kuokoa watu na mali zao hovyo malalamiko yatapungua.

"Tulikuwa tunapata shida inapotokea sehemu fulani kuna ajali ya moto, tulikuwa tukitoa taarifa lakini gari linakuja limechelewa, lakini kwa sasa litakuwa hapo hapo ofisini karibu na dereva, hata ikitokea watafanya uokoaji kwa wakati," amesema Ditrick Richard.