Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takukuru Mara yaendelea na uchunguzi miradi iliyokataliwa na Mwenge

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mara,  Hassan Mossi akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita kwa waandishi wa habari mjini Musoma.  Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa chuo cha Veta wilaya ya Butiama wenye thamani ya Sh2.21 bilioni,  mradi wa ukarabati wa chuo cha ualimu Bunda wenye thamani ya Sh762.49 milioni na mradi wa ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari ya Robanda wilayani Serengeti wenye thamani ya Sh94.38 milioni.

Musoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) mkoa wa Mara bado inaendelea na uchunguzi wa miradi iliyokataliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwkaa 2021 katika mkoa huo.

Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa taasisi yake katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, mkuu wa Takukuru mkoa wa Mara, Hassan Mossi amesema kuwa uchunguzi huo upo katika hatua za mwisho na kwamba wakimaliza watawasilisha taarifa kwa mamlaka husika.

Amesema kuwa ofisi yake ilikabidhiwa kufanya uchunguzi kwenye miradi mitatu iliyotiliwa shaka na kiongozi wa mbio za mwenge, miradi ambayo ina thamani ya zaidi ya Sh3.071 bilioni.

Mossi ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi wa chuo cha Veta wilaya ya Butiama wenye thamani ya Sh2.21 bilioni,  mradi wa ukarabati wa chuo cha ualimu Bunda wenye thamani ya Sh762.49 milioni na mradi wa ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari ya Robanda wilayani Serengeti wenye thamani ya Sh94.38 milioni.

“Tupo kwenye hatua za mwisho za uchunguzi na tukikamilisha taarifa tutapeleka kwenye channel husika kwa hatua zaidi kulingana na kitakachopatikana kutokana na huo uchunguzi huo,” amesema Mossi.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Takukuru amesema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ofisi yake ilipokea taarifa 142 ambapo kati ya hizo taarifa 42 zilikuwa zikihusu sekta ya Tamisemi hususan idara ya utawala huku taarifa zilizohusu sekta ya elimu zikiwa 17.

“Taarifa zilizohusu sekta  binafsi zilikuwa 10, ardhi tisa, afya nane, polisi na mahakama kila moja taarifa saba, maji, fedha na vyama vya ushirika vikiwa na taarifa tano na sekta zingine zilikuwa na taarifa kati ya tatu hadi moja,” amesema Mossi

Ameongeza kuwa katika kipindi hicho pia wamekamilisha uchunguzi wa majalada sita na kufungua majalada mapya saba mahakamani na kwamba taasisi hiyo ilipata ushindi katika shauri moja lililotolewa hukumu mahakamani.