Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Takwimu za pato la Taifa zinahitaji maboresho

Muktasari:

Hilo ni jambo la hatari katika nchi changa kiuchumi ambayo imekuwa ikikaribisha uwekezaji wa kampuni binafsi kutoka nchi za nje, kwa nguvu kubwa na kasi kubwa.

Tukiwa tumefikisha miaka isiyo pungua 17 tangu nchi yetu iingie  katika uchumi wa soko huria, na sekta binafsi bila mipaka bado hali ya uchumi iko vilevile kama ulivyokuwa kabla ya mwaka 1995.

Hilo ni jambo la hatari katika nchi changa kiuchumi ambayo imekuwa ikikaribisha uwekezaji wa kampuni binafsi kutoka nchi za nje, kwa nguvu kubwa na kasi kubwa.
Licha ya kuwapo maeneo mengi ya kuzungumzia, leo napenda kuchambua au kugusia eneo moja muhimu.

Kwanza, ni kuhusu tofauti zilizopo baina ya tafsiri mbili za Pato la Taifa.

Tafsiri ya kwanza, ni Pato la Taifa (GDP) ambalo ni majumuisho ya thamani ya uzalishaji wote wa bidhaa na huduma uliofanyika ndani ya mipaka ya nchi yetu katika kipindi cha mwaka mmoja  bila kutofautisha uzalishaji uliofanywa na Watanzania, na ule uliozalishwa na raia wa mataifa mengine.

Kigezo muhimu ni mipaka ya nchi na siyo uraia wa watu wanaozalisha  mali.Zipo aina tatu za kuwasilisha takwimu za pato la taifa kwa kutumia tafsiri hiyo ya kwanza.

Aina ya kwanza ni kwa njia ya pato la taifa kwa mtazamo wa vyanzo vya uzalishaji wa kiviwanda au kisekta.

Aina ya pili ni kwa njia ya pato la taifa kwa mtazamo wa aina ya matumizi kisekta. Aina ya tatu ni kwa njia ya pato la taifa kwa mtazamo wa vyanzo vya mapato.

Aina zote hizo tatu ni muhimu hasa kwa watumiaji wa takwimu hizo katika shughuli mbalimbali za kibiashara au uwekezaji nchini.

Kwa maana hiyo kukosekana kwa aina yoyote kati ya hizo ni upungufu mkubwa ambao lazima urekebishwe.
Wapo vijana wengi hivi sasa wanao hitimu shahada za uchumi na takwimu pamoja, na uhasibu  ambao wanatafuta ajira. Endapo vijana hao wakitumika kikamilifu kasoro hizo hazitokuwapo au zitapungua kwa kiasi kikubwa.

Nasema hivyo kwa kuwa kuna matatizo katika ukusanyaji wa takwimu na

Tafsiri ya pili ya Gross National Product (GNP) ambalo ni pato la taifa linajumuisha thamani ya uzalishaji wote wa bidhaa na huduma zilizofanyika nchini, lakini ambazo zimefanywa na Watanzania ndani ya nchi na nje ya mipaka ya nchi, lakini haiuhusishi uzalishaji uliofanywa na raia wa nchi za nje waliopo au waliowekeza nchini.

Kwa maana hiyo mtanzania yeyote aliyewekeza nje ya nchi, thamani ya uzalishaji wa bidhaa na huduma aliofanya katika nchi hizo hazitoingizwa katika takwimu za pato la taifa,  tafsiri ya kwanza itazingatiwa katika tafsiri ya pili ya Pato la Taifa (GNP).

Pia kwa wawekezaji nchini ambao ni raia wa nchi  nyingine duniani, takwimu za uzalishaji wa bidhaa na huduma katika viwanda au kampuni zao zilizopo nchini, hazitaingizwa katika pato la taifa kwa tafsiri ya pili (GNP) bali zitazingatiwa kwenye tafsiri ya kwanza ya Pato la Taifa (GDP).

Ni dhahiri kwamba tafsiri ya kwanza ya Pato la Taifa (GDP) kwa Watanzania haina maana sana au umuhimu mkubwa kama ilivyo tafsiri ya pili ya Pato la Taifa (GNP).

Zipo sababu nyingi , lakini hilo sio kusudio la makala haya.
Katika nchi zilizoendelea zaidi kwa viwanda duniani na ambako uwekezaji mkubwa unafanywa na raia wake, tofauti baina ya takwimu hizo mbili GDP na GNP , huendelea kupungua na kukua kidogo sana.

Kwa mfano, ukiangalia takwimu za uzalishaji wa dhahabu nchini katika kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2011, utabaini kati ya dhahabu iliyozalishwa na kuuzwa nje ya nchi ilikuwa na thamani ya dola 15 bilioni za Marekani, na Tanzania iliambulia mgao wa dola 450 milioni tu za Marekani sawa na asilimia 3 ya thamani yote ya dhahabu iliyozalishwa nchini.

(The African, 21-27 Jan.,2013) .

Mgawanyo wa aina hiyo wa mapato ya uzalishaji wa bidhaa na huduma kati ya wawekezaji wa nje na wale wa ndani upo katika maeneo mengi ya uzalishaji mali, kama katika sekta za utalii, nishati, viwanda, benki na kadhalika.

Kwa hiyo upo umuhimu mkubwa wa kukokotoa takwimu za pato la taifa katika mitazamo yote miwili GDP na GNP kwa bei za soko au za sasa, na zile za mwaka mmoja zisizo badilika.

Karibu viashiria vyote muhimu vya uchumi vinapimwa kwa kulinganisha uwiano wake na takwimu za pato la taifa.

Kutokana na hali hiyo ni muhimu kutumia takwimu za pato la taifa ambazo zinatoa taswira sahihi, na halisi wa uchumi wetu.

Kama tumedhamiria kwa dhati kukuza uchumi wetu bila kuingiza mizengwe na ubabaishaji basi hatuna budi kuwa waadilifu zaidi katika matumizi sahihi ya takwimu zenye mantiki zaidi katika mustakabali wa taifa letu.

Takwimu hizo pia zitawawezesha Watanzania kutambua ni kiasi gani cha utajiri wa rasilimali zao zinazopotea na kwenda kuzinufaisha nchi nyingine duniani.

Kwa ufahamu huo hamasa ya uwekezaji miongoni mwa Watanzania na waliopo nje utachukua sura mpya.