Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanapa yatoa askari 20 kusaidia uokoaji Hanang

Kaimu Kamishna wa Hifadhi za Taifa (Tanapa) Mussa Kuji (kulia) akizungumza na askari wanaoshiriki uokoaji kwenye maafa yaliyosababishwa na maporomoko ya tope mji mdogo wa Katesh Hanang' mkoani Manyara, baada ya kutoa Sh10 milioni na askari 20. Picha na Joseph Lyimo

Muktasari:

  • Askari watasaidia uokoaji na kusafisha mazingira ya mji mdogo wa Katesh, pia yatoa Sh10 milioni kusaidia waliokumbwa na maafa.

Hanang. Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) limetoa­ askari wake 19 na kiongozi mmoja kuungana na vikosi vingine vya uokozi katika eneo lililopata maafa kutokana na maporomoko ya matope wilayani Hanang Mkoa wa Manyara.

Pia Tanapa wametoa Sh10 milioni kuwasaidia waliokumbwa na maafa hayo pamoja na mashine moja ya kurekebisha miundombinu.

Akizungumza leo Desemba 7, 2023 Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Tanapa, Mussa Kuji amesema lengo la kupeleka kikosi hicho ni kusaidia kutoa utaalamu katika uokoaji na kurejesha miundombinu katika hali ya kawaida.

"Maafa yaliyotokea yamepoteza nguvu kazi ya Taifa na kuleta huzuni, natoa pole kwa jamii ya Katesh kwa maafa haya ambayo hayakutegemewa, kwani yamegharimu maisha ya watu na kuacha wengine wakiumia," amesema kaimu kamishna Kuji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga ameishukuru Tanapa kwa misaada hiyo, kwani imefika kwa wakati na kupelekwa kwa walengwa.

"Pia nguvu kazi ya askari 20 wa Tanapa itasaidia kuungana na majeshi mengine ya ulinzi na usalama yanayoendelea kuopoa miili na kurekebisha miundombinu ya mji mdogo wa Katesh," amesema Sendiga.

Pia amewashukuru wote walioguswa na kuchangia misaada mbalimbali.

Mmoja wa waliokumbwa na maafa hayo, Flaviana Gabriel amesema,"Tunawashukuru wote waliojitokeza kutusaidia sisi tuliokumbwa na maafa haya kwani hivi sasa hata akili zetu bado hazijakaa sawa."