TCAA kutoa mafunzo wanaotaka kutumia Drones
Muktasari:
- Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kuwajengea uwezo warushaji wa drones ili kuzijua vyema kanuni za sheria kuhusu kifaa hicho
Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, (TCAA) Hamza Johari amesema kuanzia Julai mwaka 2019 wataanza kutoa mafunzo ya kanuni kuhusu matumizi vifaa vya kielektroniki visivyo na rubani (Drones).
Johari amesema hayo leo Jumanne Juni 25, 2019 kwenye kongamano la wadau wa sekta ya anga lililoanza jana Jumatatu na kuandaliwa na TCAA, likiwa na lengo kujadili mafanikio na changamoto.
"Kozi hizi zitatolewa katika Chuo cha Mafunzo cha TCAA kilichopo uwanja wa ndege wa Terminal 1 (Dar es Salaam).Lengo la kozi hii ni wanaofanya shughuli hizi kuelewa mahitaji ya sheria ya Drones," amesema Johari.
Amesema Kanuni na matumizi ya Drones zilipitishwa Desemba mwaka 2018, lengo likiwa na lengo la kutoa mwongozo wa kisheria wa namna kufanya kwa kutumia kifaa hicho.
Mwaka 2017, TCAA ilitangaza kuwa taasisi au mtu yeyote anayehitaji kurusha drones lazima aombe kibali kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kupata ridhaa na TCAA