Teknolojia ya mtandao yakwamisha kesi ya Mbowe, kutajwa kesho

Teknolojia ya mtandano yakwamisha kesi ya Mbowe, kutajwa kesho

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi namba 63/2021 inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, baada ya teknolojia ya mtandano kwa njia ya video conference kuleta hitilafu

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, baada ya teknolojia ya mtandano kwa njia ya video conference kuleta hitilafu, kesi hiyo imeahirishwa hadi kesho Ijumaa Agosti 6.

Ni baada ya kutokea kwa hitilafu katika mfumo wa mawasiliano inayotumika kusikilizia kesi katika ukumbi wa mikutano wa video uliopo katika Mahakama ya Kisutu.

Kibatala ataja sababu za kuahirishwa Kesi ya Mbowe

Mbowe anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kula njama za kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za Ugaidi, huku wenzake watatu wakikabiliwa na mashtaka saba.


Kesi hiyo imeshindwa kuendelea leo Alhamisi, Agosti 5, 2021 kwa njia ya video kutokana na hitilafu hiyo na hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, ambaye anasikiliza shauri hilo, Thomas Simba, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 6, 2021.


Hata hivyo washtakiwa hao leo hawakuletwa mahakamani badala yake, kesi hiyo imeendeshwa njia ya mtandao.

Kabla ya kuahirisha kwa kesi hiyo,  wakili wa Serikali Mwandamizi, Pius Hila  akisaidiana na Christopher Msigwa na Grace Mwanga, ameieleza mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kutajwa.



Kwa upande wa washtakiwa wao, wanatetewa na jopo la mawakili watano ambao ni Peter Kibatala, John Mallya, Jonathan Mdeme, Fedreck Kiwelo na Sist Aloyce.


Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.


Kwa habari hii na yingine nyingine endelea kufuatilia mitandao yetu ya Kijamii.