Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tembo Seruii adaiwa kuua mtoto Kiteto

Wakati wa Kijiji cha Ndaleta, wilayani Kiteto, wakishiriki maziko ya mtoto anayedaiwa kuuawa tembo usiku wa kuamkia Septemba 16.2023. Picha na Mohamed Hamad Kiteto

Muktasari:

  • Tembo aliyepewa jina la Seurii wa hifadhi ya Tarangire, adaiwa kumuua mtoto wa miaka 10, anafahamika kwa jina la Chakutuu Lalaituu (10), ambapo inaelezwa kuwa alikanyagwa kichwani na mnyama huyo akiwa amelala.

Kiteto. Tembo aliyepewa jina la Seurii wa hifadhi ya Tarangire, adaiwa kumuua mtoto wa miaka 10, anafahamika kwa jina la Chakutuu Lalaituu (10), ambapo inaelezwa kuwa alikanyagwa kichwani na mnyama huyo akiwa amelala.

Akizungumza na Mwananchi Digital, Diwani wa Kata ya Njoro, Ramadhani Mpolonge, ameonyesha kukerwa na tukio hilo huku akiomba Serikali kuingilia kati kwani wanyama hao wamekuwa wakivamia makazi ya watu mara kwa mara.

“...bado hakuna jitihada za makusudi kupunguza madhara haya, naiomba Serikali kuingilia kati, kwani awali wayama hao (tembo), walikuwa wanavamia makazi ya watu na kula mahindi yaliyohifadhiwa, sasa wanaua watu,” amesema diwani huyo na kuongeza;

"Tumekuwa tukitoa taarifa mara kwa mara kwenye vikao vyetu juu ya madhara ya wanyama hawa lakini bado ni tatizo ni kubwa, huingia ndani ya nyumba kula mazao yaliyo hifadhiwa humo, na hapo ndipo huua, hili ni tatizo.”

Akielezea namna alivyonusuru wadogo zake wengine, Nendwalaa Lalaitoo ambaye ni kaka wa marehemu, amesema walikuwa wamelala usiku kuamkia Septemba 16, 2023; tembo huyo aliwavamia kisha kumtupia debe la mahindi alilokuwa amelalia kichwani.

Amesema baada ya kumrushia mahindi hayo, walikimbia na wadogo zake hao kuelekea porini, huku akidai kuwa kuwa wakati anafanya hivyo, tayari tembo huyo alikuwa tayari kishamkanyaga kichwani marehemu.

"Namfahamu huyu tembo akivamia nyumba huwa anataka mahindi au maji, mimi nilichofanya baada ya kuamka nilimrushia debe la mahindi nililokuwa nimelalia kichwani kisha kukimbia na wadogo zangu wengine ambao walikuwa watatu porini na wakati huo mmoja alikwisha kuawa kwa kukanyagwa kichwani," amedai kaka wa marehemu.

Kwa upande wake, Afisa Tarafa ya Olboloti, Shukumu Tuke; ambaye almwakilisha Mbaraka Batenga,Mkuu wa Wilaya hiyo kwenye maziko hayo, amewataka wananchi hao kuwa na subra, wakati mamlaka husika zinatafuta ufumbuzi wa kudumu wa suala hilo. “Mkuu wa wilaya na Mbunge wametoa pole kwa familia na wananchi, haswa kwa kaya hii iliyopata msiba huu, viongozi wameniomba niwakilishe lakini baadaye watafika kutoa pole kwa familia hii," amesema Tuke

Akizungumza kwa hisia kali Gidion Lazaro Mkazi wa kijiji hicho, amesema tembo Seurii siyo tu ni “tishio, huyu sasa anatumaliza, amemaliza mazao yetu na anatuua kwa kweli...baada ya kuua kule Kijiji cha Ngabolo, leo tena ameua hapa kwetu Ndaleta...”

Kwa mujibu wa mwananchi huyo, Seruii haogopi chochote, “wengine tunawafukuza kwa toshi, kupiga kelele lakini huyu wala hajali, hashtuki hata kidogo ndio kwanza akiona anawasogelea...ingekuwa leo tembo ndio kauawa, tungekamatwa zaidi ya watu 30 na Serikali kwa kumdhuru, lakini kwa kuwa tembo kaua mtu wala viongozi hawashtuki.”

Mawazo ya Lazaro hayapishani nay a mkazi mwenziwe katika kiki hicho aitwaye Fredi Meliyo, kwani amemueleza mwandishi wetu kuwa: "Sio kwamba Wananchi wanashindwa kumuua Seruii, hapana, sisi tunaheshimu Serikali. Japo tunawaza, kwa hali hii, tutaishije?”

“...sasa Serikali inaona mnyama ni bora kuliko maisha ya watu, kila mtu ana akili yake na anaona hali ilivyo sasa, maana haiwezekani mtu akauawa tukaendelea kuwa kimya, haiwezekani hata kidogo. Ili wananchi tusifanye lolote, Serikali ituondolee hawa wanyama karibu na makazi yetu,” amesema Meliyo.

Mkazi huyo amesisitza kuwa: “Kwa kuwa wafugaji wameondolewa maeneo yenye wanyama wakali huko Tarangine, na sasa wanyama hao wanatufuata kwenye makazi yetu na kufanya uharibifu na hata kuua, Serikali isione maisha wanyama pori ni muhimu kuliko maisha yetu, nasema hatutakubali."