Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tembo wajeruhi wawili akiwemo mtoto wa miaka sita

Muktasari:

  • Hofu imetanda katika kata ya Mdimba na kata ya Chingungwe Wilayani Tandahimba baada ya tembo watatu kuonekana na kujeruhi watu wawili huku wengi wakijiuliza wapi

Mtwara. Hofu imetanda baada ya watu wawili kujeruhiwa na mnyama tembo katika wilaya ya Tandahimba ambaye ni Faraji Rahisi (30) na mwingine ni mtoto wa miaka sita ambaye alikuwa nje ya nyumba yao.

Akizungumzia na Mwananchi kwa njia ya simu  Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patrick Sawalla alisema kuwa watu hao waliojeruhiwa wanatoka katika vijiji viwili tofuati.

“Kwa kweli tembo hawajawahi kusikika katika wilaya yetu yaani hata sisi tunashangaa tunasubiri taarifa ya TAWA ili tuweze  kujua wametoka wapi”

“Lakini tumetoa rai kwao kwakuwa tumeambiwa na watalaamu kuwa tembo hawataki kelele hivyo tumewasihi wakae majumbani wasipige kelele wala wasiwarushie mawe kwakuwa hawapendi kelele lakini mashairika mbalimbali yapo huko yanatoa elimu ili wananchi wanachukue tahadhari” Kanal Sawalla

Nae Diwani wa Kata ya Chingungwe  Juma Hamisi Mdiliko  alisema kuwa katika kata yake ni mtu mmoja aliyejuruhiwa ambaye anajulikana kwa jina la Faraji Ismail Rahisi(30) ambapo alikuwa shambani akiendelea na majukumu yake.

“Alikuwa peke yake analima kwakuwa  mashamba yetu tumepakana pakana hivyo baada ya kulia ndio majirani wakakimbilia huko na kutoa taarifa kwetu serikali ya kijiji na tukamchukua na kumuwahisha katia kituo cha afya Mahuta ambapo alipata huduma ya kwanza kisha kupelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Tandahimba”

“Sisi hatuko karibu na hifadhi yoyote ndio maana tunashamba kikubwa tunaomba tujue wametokea wapi na elimu itolewe juu ya tembo ili wananchi wajue namna bora ya kujilinda nao kwasasa wamekosa amani”

Nae Mkazi wa Kijiji cha Mdimba Jazal Salum Namchenda alisema kuwa mgonjwa huyo ni ndugu yake na anaendelea vizuri kabla ya tukio alikuwa analima asubuhi saa moja ndio alitokea tembo na kumjeruhi.

kwa mujibu wa mgonjwa hakumuona tembo ila mkewe alikuwa shambani japo mbali lakini alimuona tembo alipojaribu kumwambia mumewe lakini hakumuelewa ndio akajeruhiwa”

“Hatujui tembo katoka wapi hatujawahi kusikia Tembo katika maeneo yale hata sisi tumeshangaa lakini tunahsukuru mgonjwa wetu anaendelea vizuri na leo ameamka salama na amekula chakula bila tatizo