Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tembo wazuia wanafunzi kwenda shule, waua wananchi wawili

New Content Item (1)

Wananchi kijiji cha Mangae wilayani Mvomero  wakichimba kaburi kwa ajili ya kuzika miili ya watu wawili walifariki kwa kukanyangwa na tembo . Lilian Lucas.

Muktasari:

  • Wingi wa tembo kwenye maeneo mbalimbali nchini umekuwa tishio kwa wananchi na kuwafanya kuacha kufanya shughuli za maendeleo.

Morogoro. Watu wawili wakazi wa vitongoji vya Makang'wa na Shule, Kata ya Mangae Wilayani Mvomero wameuawa na tembo kwa nyakati tofauti wakati mmoja akipita njia kuelekea shambani na mwingine akiokota kuni, huku wanafunzi wakishindwa kwenda shule.

Waliofariki dunia ni Thelesphory  August (25) mkazi wa Kitongoji cha Shule aliyekuwa akipita njiani kwenda shambani na Leah Lipasio Lekole (45) mkazi wa Kitongoji cha Makang'wa aliyekuwa ameenda akiokota kuni kwa ajili ya shughuli za nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mangae, Belege Alex amekiri kutokea kwa matukio hayo Novemba 9, 2023 na kwamba matukio hayo yametokea Novemba 7 mwaka huu huko Kijiji cha Mangae wilayani Mvomero mkoani Morogoro kuanzia saa 5.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.

Alex amesema matukio hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na ni endelevu pamoja na Serikali kuendelea kuwahimiza wananchi kuendelea kuwa waangalifu wakati wote.

Amesema Thelesphory akiwa anaenda kwenye shughuli zake za kawaida shambani Novemba 7 mwaka huu  saa 5.00 asubuhi alikanyangwa na tembo na mwili wa marehemu ulihifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro.

“Mwili wa mama Leah alipopatwa na tatizo la kukanyangwa na tembo hatukumpata wakati huo tumemuona asubuhi na sasa tunawahifadhi ndugu zetu wawili. Serikali ya kijiji tumekuwa tukichukua tahadhari mbalimbali lakini bado hali ni mbaya kwani kila siku wanayama hawa wanaongezeka na kuleta madhara,”amesema.

Alex amesema mpaka sasa tangu tembo hao waanze kuingia kijiji hapo pekee watu 19 wamefariki kutokana na tembo na wamekuwa wakifanya vikao mbalimbali na mkuu wa wilaya wataalamu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa), pamoja na Shirika la Uhifadhi Tanzania (Tanapa).

“Haya ni matukio endelevu jitihada za serikali nado sio nzuri na haya ni matukio ya tangu mwaka 2013,”amesema mwenyekiti huyo wa kijiji.

Theresia Maruganje mkazi wa Kitongoji cha Makang'wa, Kata ya Mangae, amesema kwa muda mrefu kijijini hapo kumekuwa na changamoto ya tembo na kwamba kwa sasa wamekuwa wakishindwa kwenda kukata kuni, watoto hawaendi shule na kuchota maji kwa ajili ya huduma zao.

Amesema marehemu Leah alitoka nyumbani kwake kwenda kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia watoto wake ambao ni walemavu na kama wananchi wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo kwa kuhofia tembo na kwamba tembo wamezagaa na wengi kwenye maeneo yao.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mlinge Joseph Masingisa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mazishi ya marehemu hao alisema tukio hilo la kuuawa na tembo kwa wananchi hao lilitokea Novemba 7 mwaka huu, marehemu Leah alienda kukata kuni na kukutana na tembo na kuanza kumshambulia na kufariki.

“Unaweza kukutana na kundi la tembo kuanzia mia, mia mbili, watu wamekuwa waoga hadi wanafunzi wakiwa wanatoka shuleni wanawafuata, hapa Mangae kila mwaka watu wanakufa,” amesema

Ameiomba serikali kufatilia na kuweza kuwadhibiti tembo hao kwani kwa sasa shughuli zimekuwa hazifanyiki na usalama ni mdogo kwao, watu hawalimi, hawaendi kuchota maji.

Kaka wa marehemu Leah, Mainaya Lupasho amesema familia walipata taarifa ya dada yake kuwa ameenda kukata kuni mchana na baadaye wakasikia kuwa hajarudi nyumbani mpaka saa kumi na mbili jioni wakaanza kuuliza kwa majiradi lakini walieleza hawajamuona.

Lupasho amesema wakaelezwa kuwa kuna tembo alipiga kelele na mtu alisikika akipiga kelele, marehemu alionekana ameumizwa maeneo ya mbavu.

Kitongoji cha Makang'wa kiko umbali wa zaidi ya kilometa tano kutoka barabara kuu ya Morogoro kwenda Iringa na waandishi wa habari walifika na kushuhudia wananchi wakiendelea na shughuli za mazishi, huku askari wa jeshi la polisi, Tawa pamoja na wale wa Tanapa hifadhi ya mikumi wakiwa maeneo hayo.