TMDA yawataka wafamasia kudhibiti bidhaa zilizoisha muda wa matumizi

Muktasari:

  •  Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Kanda ya Kusini imewaasa wafamasia mkoani mtwara kudhibiti bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi katika vituo vya kutolea huduma.


Masasi. Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Kanda ya Kusini imewaasa wafamasia mkoani mtwara kudhibiti bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi katika vituo vya kutolea huduma.

Akizungumza katika kikao kazi cha wafamasia kutoka halmashauri zote za mkoa huo, Meneja wa TMDA-Kanda ya Kusini, Engelbert Mbekenga amesema ni vyema kuwa karibu na TMDA ili kuweza ku kuteketeza bidhaa hizo ambazo ni hatarishi kwa binadamu na mazingira.

 “Fanyeni kaguzi kwenye maeneo yanayotoa huduma za afya kama maduka ya dawa, maabara, zahanati, vituo vya afya na hospitali lengo likiwa ni kuangalia usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa upande wabinadamu na mifugo”

“Washiriki natambua kwamba Dawa na VifaaTiba vinaweza kuleta madhara katika matumizi ya kawaida ya kila siku sasa niombe uwajibikaji wa kutosha katika utoaji wa taarifa za madhara yanayoweza kutokea mara baada ya mteja kutumia Dawa au kifaa tiba” 

Kwa upande wake Mkurugenzi waHalmashauri ya Mji wa Masasi, Elias Ntiruhungwa amesema ni jambo la busara tumbaku kupata mamlaka ya kuidhibiti itasadia jamii kuwa na uelewa wa madhara ya matumiiz ya bidhaa hiyo.