Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tucta yaitoa hofu sekta binafsi nyongeza mishahara

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Henry Mkunda.

Muktasari:

  • Kutokana na maoni ya kutaka sekta binafsi isiachwe nyuma katika nyongeza za mishahara zinazotangazwa, Katibu Mkuu Tucta Henry Mkunda amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Henry Mkunda amesema sekta binafsi haijasahaulika katika nyongeza ya mishahara, kwani wameomba iundwe bodi ya kima cha chini cha mishahara ili ifanye utafiti na kujiridhisha kuwa kiwango kitakachopangwa.

 Ametoa kauli hiyo ikiwa ni baada ya wachangiaji wa Mwananchi Twitter space kupaza sauti kutaka sekta binafsi ikumbukwe katika nyongeza za mishahara zinazotangazwa.

Mada iliyojadiliwa leo, Mei 3, 2023 ilikuwa ikisema Nini maoni yako juu ya hotuba ya Rais Kuhusu maslahi ya wafanyakazi nchini.

"Si kwamba tumeiacha sekta binafsi, tunaomba iundwe bodi ya kima cha chini cha mishahara ili ifanye tafiti na kujiridhisha kiwango kitakachopangwa kitaendana na uhalisia wa maisha," amesema Mkunda.


Awali akichokoza mada, Kaimu mhariri wa uchumi gazeti la Mwananchi, Ephrahim Bahemu amesema Serikali katika kurejesha nyongeza ya mshahara kila mwaka inapaswa kuangalia pia na sekta binafsi kwani watu wote wanaoshi katika mazingira ya aina moja ambayo gharama zake zinaongezeka.

Maneno yake yaliungwa mkono na Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU), Paul Loisulie aliyeshauri kuwa katika maadhimisho ya sikukuu ya wafanyakazi mwaka ujao, nyongeza za mshahara zifanywe kwa sekta zote yaani ile ya umma na Sekta Binafsi.

Hiyo ni kutokana na kile alichoeleza kuwa Serikali ni mlezi wa sekta zote hivyo inatakiwa pia kushughulikia upande wa sekta binafsi.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Nasikiwa Berya amesema kama shirika litaendelwa kutoa ushirikiano kwa Serikali na wadau wake katika kutekeleza mipango kazi yenye staha na kuimarisha haki za msingi.

 "Tuko tayari kuendelea kutoa elimu kwa Serikali na wanachama mbalimbali tuna milango yetu iko wazi karibuni tuone ni kwa namna gani tuendelee kufanya kazi pamoja."