Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Muktasari:

Kwa Paul Makonda, aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mwaka 2020 umekuwa pigo kwake. Alipoteza ukuu wake akiutaka ubunge alioukosa.

Kwa Paul Makonda, aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mwaka 2020 umekuwa pigo kwake. Alipoteza ukuu wake akiutaka ubunge alioukosa.

Makonda, kijana aliyeonekana kama mwana mpendwa wa Rais John Magufuli hata kudhaniwa asingeachwa, alitia nia kugombea Jimbo la Kigamboni lakini wajumbe wa CCM hawakumpa nafasi. Badala yake, mbunge wa mihula miwili wa jimbo hilo na waziri wa Tehama sasa hivi, Faustine Ndugulile, akapitishwa.

Kwa Taifa, mwaka 2020 ulikithiri maumivu. Watu ambao ni hazina kwa nchi, wameondoka hivyo kupunguza visima vya hekima na maarifa ya uongozi.

Tangu Oktoba 1999, alipofariki Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Tanzania haikutikiswa kwa msiba mkubwa kama mwaka 2020.

Kutoka Oktoba 14 ya mwaka 1999 hadi Julai 24 mwaka huu ni zaidi ya miaka 20, Tanzania imempoteza Rais Benjamin Mkapa, aliyeliongoza Taifa kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005.

Mkapa, alianza utumishi wa umma kama katibu tawala wilayani Dodoma, akawa ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje kisha mhariri wa magazeti ya chama (Tanu) na Serikali, kabla ya kuwa ofisa habari wa Rais Nyerere. Alipanda mpaka akawa balozi, waziri hatimaye Rais wa Tanzania.

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Kwa uzoefu wake, Mkapa alikuwa hazina kubwa kwa nchi. Alihitajika kutoa mwongozo kwa viongozi wa kizazi kipya. Yeye ni mmoja wa viongozi wachache waliofanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Nyerere.

Julai 7, saa 11 asubuhi katika Hospitali ya Mliganzila, Job Lusinde, waziri pekee aliyekuwa amebaki katika baraza la kwanza la mawaziri la Tanganyika, alivuta pumzi yake ya mwisho.

Lusinde, mbali na uwaziri, alikuwa balozi wa Tanzania nchini China kisha Kenya halafu akawa mwenyekiti wa bodi ya Tanapa. Alikuwa alama pekee ya Baraza la Mawaziri la Mwalimu Nyerere.

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Mwanasheria mkuu wa Serikali wa kwanza Mtanzania, Jaji Mark Bomani, alivuta pumzi yake ya mwisho Septemba 10. Bomani alilitumikia Taifa katika maeneo mengi ikiwamo kuiongoza Tume ya Madini.

Augustino Ramadhani, jaji mkuu wa Tanzania kati ya mwaka 2007 na 2010 na jaji mkuu wa Zanzibar mwaka 1978 hadi 1989 alifariki Aprili 28.

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Jaji Ramadhani alikuwa makamu mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba. Alihudumu pia kama makamu mwenyekiti wa Tume wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Mpaka mwisho wa uhai wake, Ramadhani alikuwa mchungaji wa Kanisa la Anglikana licha ya kulitumikia Jeshi la Wananchi mpaka ubrigedia jenerali enzi za uhai wake.

Mwanadiplomasia nguli, Augustine Mahiga aliaga dunia Mei Mosi akiwa Waziri wa Katiba na Sheria. Dk Mahiga alikuwa balozi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

Pigo bungeni

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Dk Mahiga ni kati ya wabunge waliopoteza maisha wakiendelea na utumishi. Aprili 20, Gertrude Rwakatare, alifariki akiwa mbunge wa Viti Maalum na mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mikocheni B Assemblies of God.

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Aprili 29, aliyekuwa mbunge wa Sumve, Richard Ndassa, naye alifariki. Hawa wawili wlaipoteza maisha baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa Newala Vijijini, Rashid Ajali Akbar, kilichotokea ghafla Januri 15 huko Mingoyo, Lindi.

Septemba 14, wananchi wa Jimbo la Mpendae, Zanzibar walimpoteza mbunge wao wa mihula miwili, Salim Turky. Wakati anafariki Turky alikuwa kwenye kampeni za kuwania muhula wa tatu.

Kudhihirisha ushawishi wake, baada ya kifo cha Turky, mwanaye Toufiq, alidhaminiwa na CCM kugombea nafasi hiyo na sasa ndiye mbunge wa Mpendae.

Wengi hawajamsahau Turky kwa moyo wake wa upendo na ukarimu hasa aliposhiriki kuokoa maisha ya Tundu Lissu, aliyepigwa risasi Septemba 2017. Turky ndiye aliyekodi ndege iliyomsafirisha Lissu kwenda Nairobi, Kenya.

Tamthiliya ya kisiasa

Kuondoka kwa Makonda ni sehemu ya tamthiliya ndefu ya siasa iliyochukua nafasi mwaka huu. Ni kama Waziri Mkuu wa zamani, Fredrick Sumaye, alivyoamua kurejea CCM licha ya viapo alivyovitoa huko nyuma.

Kutimuliwa uanachama wa CCM kwa waziri wa zamani wa mambo ya nje, Bernard Membe kisha kujiunga ACT-Wazalendo halafu kugombea urais, kulitengeneza uhusika wa aina yake katika tamthiliya ya kisiasa mwaka huu.

Ulikuwa mwaka wa tamthilia za kisiasa, misiba mikubwa nchini

Membe hakufanya kampeni ila akatamba kuwa angeingia kutokea benchi dakika ya 89 na kufunga bao la ushindi. Lakini akabaki kimya. Uchaguzi ulipomalizika, akaomba radhi kwa mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli na chama chake cha zamani akiahidi kurejea Januari mosi mwakani. Alitumia ukurasa wake wa Twitter kusema haya.

Tundu Lissu, ndiye mhusika mwenye nguvu katika tamthiliya ya kisiasa mwaka huu. Kurejea kwake nchini kulitikisa licha ya kutokuwapo kwa takriban miaka mitatu tangu alipopigwa risasi Septemba 2017.

Lissu aligombea urais kupitia Chadema katika mazingira ambayo wengi waliamini asingekubaliwa kwani hata kwenye chama chake, kulikuwa na mvutano. Kwa hisia, iliaminika angezuiwa kwa sababu ya kesi alizokuwa nazo mahakamani.

Mivutano yake na Jeshi la Polisi kipindi cha kampeni kiasi cha NEC kumsimamisha kufanya kampeni kwa wiki moja na namna alivyoomba hifadhi ubalozi wa Ujerumani nchini kabla hajaondoka kwenda Ubelgiji chini ulinzi wa kibalozi, ni sehemu iliyovuta hisia za wengi kwenye tamthiliya ya kisiasa mwaka huu.

Habari za kufutwa kwenye orodha ya mawakili zilimfanya Fatma Karume kuwa mwanamke aliyetajwa na kutikisa mwaka 2020.

Mwanasheria mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi alimshitaki Fatma kuhusu matumizi ya mitandao hasa Twitter kuwa ni kinyume na maadili ya uwakili na uofisa wa Mahakama Kuu. Fatma ni mwanasheria msomi aliyekuwa rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

Halima Mdee na wenzake 18 wametengeneza uhusika wa aina yake mwaka huu. Wao walienda bungeni kuapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum kinyume na msimamo wa chama chao, Chadema.

Licha ya Halima, wengine walioapa ni Grace Tendeka, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambat, Nusrat Hanje, Jessica Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.

Walikuwapo pia Asia Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Halima, mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na wenzake walitimuliwa uanachama ila wakaahidi kukata rufaa ingawa hawajaiwasilisha mpaka sasa.

Freeman Mbowe na viongozi wengine waandamizi Chadema, walihukumiwa kwenda jela miezi mitano kwa kila kosa baada ya kukutwa na hatia katika makosa 12. Vinginevyo, Mbowe na wenzake walitakiwa kulipa faini, jumla ya Sh350 milioni. Walilipa faini kuepuka jela.

Wengine kwenye hatia hiyo inayohusiana na kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini kilichotokea Februari 16 mwaka 2018, ni katibu mkuu Chadema, John Mnyika, naibu katibu mkuu Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu na aliyekuwa mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.

Alikuwamo pia katibu mkuu wa zamani wa Chadema, Vincent Mashinji, wabunge wa Viti Maalum, Halima Mdee, Ester Bulaya na Esther Matiko.

Michango iliyotolewa iliwatoa jela viongozi wa Chadema isipokuwa Mashinji ambaye alikuwa amehamia CCM hukumu ilipotolewa, faini yake ililipwa na katibu wa itikadi na uenezi CCM, Humphrey Polepole.

Tamthiliya ya kisiasa inaongezewa uhusika na pigo la wabunge mahiri wa upinzani, Zitto Kabwe, Godbless Lema, Mbowe, Msigwa, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu na wengine, kupoteza nafasi zao katika mazingira yaliyoacha maswali mengi.

Baada ya kukosa ubunge, Lema alilalamikia usalama wa maisha yake, akaomba hifadhi Kenya kabla ya kupewa haki ya kuwa mkimbizi nchini Canada, yeye na familia yake.

Naibu katibu mkuu wa ACT-Wazalendo, Nassor Mazrui alibamba mitandaoni alipotoweka kabla haijabainika kuwa mikononi mwa polisi. Mazrui alihusika vyema katika tamthiliya ya kisiasa kutoka Zanzibar.

Ismail Jussa, mmoja wa viongozi waandamizi wa ACT-Wazalendo, alipigwa na kuumizwa kisha kusafirishwa hadi Nairobi kwa matibabu. Uchaguzi ulimalizika Zanzibar na roho za watu kadhaa kutokana na ghasia zilizojitokeza.

Hata hivyo, tamthiliya iliacha mshangao Pemba, iliko ngome ya upinzani tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Katika majimbo 18 ya Pemba, CCM walipata 14, ACT-Wazalendo manne.

Kwa Zanzibar, tamthiliya ya kisiasa iliisha kwa mapatano ya CCM na ACT-Wazalendo kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Mwenyekiti wa ACT, Maalim Seif Sharif Hamad ameteuliwa kuwa makamu wa kwanza wa Rais.