Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upelelezi kesi ya aliyekuwa kocha Simba waendelea


Muktasari:

Muharami na wenzake, wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za Kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 34.89.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa upelelezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa kocha wa makipa wa timu ya Simba Sport Club, Muharami Sultan (40) na wenzake watano, bado haujakamilika.

Sultani na wenzake, wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za Kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 34.89.

Wakili wa Serikali, Caroline Materu, ameieleza mahakama hiyo leo, Desemba 5, 2022 wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 71/2022 ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Matemu amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio kuwa washtakiwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mrio, baada ya kusikiliza maelezo ya upande wa mashtaka, ameahirisha kesi huyo hadi Desemba 19, 2022 itakapotajwa.

Hata hivyo, washtakiwa hao hakupelewa mahakamani hapo isipokuwa kesi hiyo imeahirishwa kwa njia ya video, huku washtakiwa wakionekana kwenye video kupitia luninga iliyowekwa katika ukumbi wa mikutano wa Mahakama ya Kisutu.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa kwa pamoja walifikishwa mahakamani hapo Novemba 21, 2022 wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya.

Mbali na Sultani, washtakiwa wengine ni mmiliki wa kituo cha Cambiasso Sport Academy kilichopo Tuangoma, Kambi Zubery Seif, Said Matwiko mkazi Magole, Maulid Mzungu maarufu mbonde, mkazi wa kisemvule, John John (Chipanda) mkazi wa Kitunda na Sarah Joseph.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa Oktoba 27, 2022 eneo la Kivule jijini Dar es Salaam kwa pamoja walisafirisha dawa za Kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 27.10.

Pia, Novemba 4, 2022 maeneo ya Kamegele Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, washtakiwa hao kwa pamoja walisafirisha dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo 7.79.

Washtakiwa wapo rumnde kutokana na mashtaka yanayowakabili hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.