Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uzee wakatisha uhai wa faru Rajabu

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Rajabu, faru maarufu zaidi nchini aliyeishi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), amefariki akiwa na miaka 43.


Arusha. Rajabu, faru maarufu zaidi nchini aliyeishi katika Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), amefariki akiwa na miaka 43.

Faru huyo ambaye ni mtoto wa faru John aliyekufa mwaka 2015, alizaliwa Ngorongoro mwaka 1979 na mwaka 1993 akahamishiwa Hifadhi ya Serengeti.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Paschal Shelutete amesema kama ilivyo kawaida za uhifadh, wanaangalia namna bora ya kuuhifadhi mwili wake.

Wakati faru Rajabu akiacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa, baba yake, faru John alikufa kutokana na tabia yake ya ugomvi kwa madume mengine aliowajeruhi huku naye wakimwachia vidonda.

Faru John alikufa akimwacha mtoto mmoja tu, faru Rajabu ambaye alijizolea umaarufu kutokana na jitihada kubwa alizozifanya kuongeza uzao wake kiasi cha kupongezwa na Hayati Rais John Magufuli kwa kuongeza idadi ya faru eneo la ikolojia ya Serengeti na kufikia hatua ya kuombwa katika hifadhi nyingine.

Faru ni miongoni mwa wanyama walio hatarini kutoweka duniani hivyo umahiri wa faru Rajabu ulikuwa faraja katika uhifadhi wa viumbe hao sio Tanzania pekee bali duniani kwa ujumla.

Faru wapo hatarini kutoweka duniani kutokana na uwindaji haramu unaofanywa ili kuvuna pembe zao licha ya biashara hiyo kupigwa marufuku maeneo mengi.

Pembe za faru zinaotumika zaidi katika nchi za Asia kama tiba ya magonjwa huku zikidaiwa kuimarisha nguvu za kiume, ni biashara haramu inayopingwa lakini bei kubwa ya pembe hizo inawafanya majangili washindwe kuiacha.

Kilo moja ya pembe za faru huuzwa kwa takriban dola 65,000 za Marekani (Sh40 milioni). Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyodhibiti ujangili wa faru.