Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vijana 1,000 kunufaika na ufadhili wa mafunzo

Muktasari:

  • Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa, Adolf Mkenda ameagiza uchaguzi wa vijana watakaonufaika na ufadhili wa mafunzo ya ujuzi kuwa wazi.

Dodoma. Vijana 1,000 watanufaika na ufadhili wa mafunzo ya ujuzi yatakayotolewa kwenye vyuo vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Veta), ikiwa ni hatua za kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, amesema leo Alhamis Julai 20, 2023 wakati akisaini mkataba wa ufadhili wa mafunzo hayo na uongozi wa VETA.

Sabi amesema suluhisho la ukosefu wa ajira nchini ni kutengeneza mazingira bora yatakayowezesha vijana wengi kujiajiri, kwenye ajira stahiki zitakazowawezesha kujipatia kipato.

“Jambo hili litawezekana kupitia shughuli za ufundi stadi, shughuli kwenye sekta ya teknolojia ama shughuli zinazohusu ubunifu na mengine. Mafunzo yatakayowawezesha vijana kuwa mahiri katika maeneo haya ndio mkombozi wa tatizo la ajira kwa vijana,”amesema.

Amesema ndio maana kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wameamua kuanzisha mpango wa ufadhili wa ufundi stadi kwa vijana kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo Stadi (Veta).

Sabi amesema mpango huo unajulikana kwa jina la NBC Wajibika Scholarship, ambao utalenga kutoa ufadhili kwa vijana 1,000 na kwamba wametenga Sh100 milioni kwa kuanzia.

Amesema kupitia fedha hizo watafundishwa masomo ya ufundi ujenzi, ushonaji, useremala, upambaji na mengineyo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amewataka kutokuwa na hofu kwasababu fedha hizo zitatumika kwa uadilifu na kwa uwazi.

“Na sisi vitabu vyetu vitakuwa wazi muda wote kuona utaratibu ambao tutautumia. Lakini tungependa utaratibu huu uwekeze katika fani moja ikiwezekana chuo kimoja ama viwili, tuweze kupima matokeo makubwa kwa miaka miwili ama mitatu,” amesema.