Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadaiwa kumshambulia baba wa kambo

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, linachunguza kisa cha kukatwa mapanga kwa mkulima Salehe Rashidi, ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Makangaga, Wilaya ya Kilwa; mkoani hapa, na watu wanaodaiwa kuwa ni watoto wa mke wake.

Lindi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Lindi, linachunguza kisa cha kukatwa mapanga kwa mkulima Salehe Rashidi, amba ye ni mkazi wa Kijiji cha Makangaga, Wilaya ya Kilwa; mkoani hapa, na watu wanaodaiwa kuwa ni watoto wa mke wake.

Akiongea na Mwananchi Digital, Kamanda wa jeshi hilo mkoani Lindi, Pili Mande; amekiri kupata taarifa za tukio hilo huku akisema: “Tunaendelea na uchunguzi.”

Kwa mujibu wa RPC Mande, tukio hilo limetokea August 30 mwaka huu saa 7: 00 mchana, wakati Rashid alipokuwa shambani kwake akilinda mazao yasishambuliwe na wanyama waharibifu, ndipo alipofuatwa na vijana hao na kushambuliwa.

Kwa upande mwingine, Rashid amefafanua pale alipoongea na mwandishi wetu kuwa: “Nilikuwa shambani nikilinda mazao, ghafla wakatokea watuhumiwa wakiwa na mapanga na fimbo mikononi mwao.”

Kwa mujibu wa mhanga huyo, watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa, ambapo kwa pamoja walianza kumshambulia, huku kijana mmoja akimkata na panga kwenye mguu na baadaye mkono wa kulia, na mwingine akimsahambulia kwa fimbo kichwani.

“Sababu ya shambulio hili ni kitendo cha mimi kuwataka warejeshe vitu walivyochukuwa wamechukua nyumbani, kikiwemo kitanda, suala ambalo hata mama yao analifahamu,” amesema mkulima huyo na kuongeza;

“Baada ya kumaliza kunishambulia, nasikia walienda Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji, na kueleza wenyewe kile walichokifanya, baadaye ndugu walifika na kunipeleka Zahanati ya Kiranjeranje, lakini kutokana na uzito wa tatizo, nikaletwa Hosptali ya Mkoa Sokoine.”

Mama mzazi wa vijana hao Ashura Abdallah, amesema kitendo walichokifanya watoto wake si cha kiungwana na kuomba Serikali ichukue hatua kali japo ni watoto wake.

"Kitendo hiki sijakipenda kabisa, kama wameweza kumfanyia hivi baba yao wa kambo, ipo siku hata mimi wanaweza kinidhuru, ninaiomba Serikali kuchukua hatua stahiki kwa hawa watoto, kiukweli sina amani na hawa watoto wangu,” amesema Ashura.

Mganga Mfawidhi hospitali hiyo, Dk Alexander Makalla, amethibitisha kumpokea mgonjwa huyo Agosti 30, 2023 saa 2:00 usiku.

Dk Makalla amesema mgonjwa huyo ameshambuliwa na kitu chenye kali mguu na mkono wa kulia na kichwani, hata hivyo, hali yake inaendelea vizuri kutokana na huduma za matibabu anayoyapata.