Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wataja vikwazo kuanzisha biashara nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza akizungumza wakati wa mkutano uliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Liberty Sparks chini ya ufadhili wa Atlas Network kwa lengo la kujadili maeneo yanayopaswa kuangaliwa nchini ili kuboresha mazingira ya kibiashara.

Muktasari:

Wadau masuala ya biashara wameeleza kuwa vikwazo vinavyowakwamisha watu kuanzisha biashara ni ucheleshwaji wa usajili wa kampuni na upatikanaji wa vibali kutoka mamlaka zinazohusika na utoaji wa vitu hivyo.

Dar es Salaam. Wadau masuala ya biashara wameeleza kuwa vikwazo vinavyowakwamisha watu kuanzisha biashara ni ucheleshwaji wa usajili wa kampuni na upatikanaji wa vibali kutoka mamlaka zinazohusika na utoaji wa vitu hivyo.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza wakati wa mkutano uliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Liberty Sparks chini ya ufadhili wa Atlas Network kwa lengo la kujadili maeneo yanayopaswa kuangaliwa nchini ili kuboresha mazingira ya kibiashara.

Hamza amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali bado kuna changamoto nyingi katika uanzishaji wa biashara ikiwemo ya muda unaotumika kwa mtu anapotaka kusajili kampuni kwa ajili ya kuanza kufanya biashara.

Amesema siku 28 zinazotumika mpaka mtu kupata usajili wa kampuni bado ni nyingi hivyo wanaziomba mamlaka husika zirekebishe ili ziwe chini ya hapo kwa lengo la kurahisisha uanzishwaji wa biashara.


"Ripoti ya Dunia imeonesha wazi kuwa bado kuna changamoto hasa katika mtu kuanza biashara, mtu akitaka kuanzisha kampuni inachukua siku 28 siku ambazo ni nyingi, tutumie mifumo ya teknolojia kurahisisha jambo hili," amesema na kuongeza

"Pia tunashauri kuboreshwa kwa mchakato mzima wa urasimishaji biashara ili kuweza kuwa na biashara nyingi ambazo ni rasmi zitakazowafanya wafanyabiashara kupata faida zaidi na kuweza kupata watu wa kuwekeza nao katika biashara nao," amesema

Amesema wanaona namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan anavyofanya jitihada za kuifungua nchi jambo ambalo amefanikiwa katika nchi nyingi hivyo ili wafanyabiashara wanufaike na fursa hiyo hawana budi biashara zao kuwa rasmi.

Mwakilishi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Eliabu Rwabiyagi amesema kwa sasa Serikali imejitahidi kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na kurahisisha taratibu za uazishwaji wake.

Amesema kwa upande wa Brela wana mfumo mpana wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS) ambao unatoa huduma zote kwa mtandao ikiwemo usajili wa kampuni, majina ya biashara pamoja na alama za biashara.

“Hivyo watu ambao wanasema wanachukua muda mrefu kupata huduma zetu si kweli kwani mambo kupitia mtandao yamerahishwa sana, mfumo wetu unamuwezesha mtumiaji kupata huduma popote alipo wakati wowote bila kulazimika kufuata huduma hizo katika ofisi za Brela,” amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Liberty Sparks, Evans Exaud amesema wanachofanya sasa ni kuangalia urahisi wa ufanyaji biashara nchini kwa kuangalia nchi zingine zinafanyaje na ni kwa jinsi gani wataweza kupata mapendekezo yatakayosaidia Tanzania nayo kufanya vizuri katika eneo hilo.

Amesema wameamua kukutana na taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi ambazo zimekuwa zikijihusisha na masuala ya biashara kwa lengo la kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike kwenye ufanyaji wa biashara ili kuweza kupunguza umasikini na kuongeza ajili kwa watu.