Wahitimu wa fani ya utalii watakiwa kutumia 4R

Wahitimu wa Chuo Cha Taifa cha Utalii Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maliasilina Utalii, Balozi Pindi Chana kwenye sherehe ya mahafali ya 22 ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam.
Muktasari:
- Wahitimu Chuo Cha Taifa Cha Utalii watakiwa kutumia falsafa ya4R katika kuwahudumia wateja kwenye maeneo yao ya kazi
Dar es Salaam. Wahitimu wa 595 wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania, wamehimizwa kwenda mifanya shughuli zao kwa kuzingatia falsafa 4R katika utoaji huduma ikiwa ni njia nzuri ya kutengeneza ukarimu.
Vilevile,wametakiwa kuangalia fursa kwa kuzingatia mahitaji ya soko,ikiwemo kujifunza lugha mbalimbali na kujua namna ya kuaanda vyakula vyao na kuwahudumia ipasavyo ili kuendana na uhalisia wa thamani ya fedha wanayotoa.
Hayo,yalisemwa na Dar es Salaam Leo,Desemba 6,2024 na Waziri wa Maliasiri na Utalii,Balozi Pindi Chana alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 22 ya chuo na kutoa vyeti kwa wahitimu 595 wa Astashahada na Shahada ya Utalii na uratibu matukio pamoja na Ukarimu.
"Niwapongeze kwa kuhitimu mkatuwakilishe vyema huko muendako nimesikia mmeshapata ajira sasa katika kufanya kazi zenu mkazingatie kutumia falsafa ya 4R iliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wateja wenu," amesema
"Inatakiwa pia mjua namna ya kuandaa na kupika vyakula vyao kwa ufasaha na hata huduma mnazowapa inatakiwa ziwe na sifa stahiki kwa kuzingatia thamani ya fedha wanazotoa," amesema Balozi Chana
"Serikali tumejipanga kuendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi na kama mnavyojua kuna Samia Scolaship ambayo hata chuo hiki kinanufaika katika kuendeleza wanafunzi mkipata fursa itumieni," amesema
Amesema sekta ya utalii kwa sasa inatija kubwa kwani mchango wake katika pato la Taifa ni asilimia 17 na katika kuingiza fedha za kigeni ni asilimia 25.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Imani Kajula amesema kuna rekodi utalii unaongezeka kwenda juu ikichagizwa na sera nzuri.
"Dunia ya leo ina mambo makuu matatu, kujifunza lugha,kufanya utafiti na ujasiriamli ni nguzo muhimu katika kufanikiwa kupata ajira," amesema
Awali, Mkuu wa Chuo hicho,Dk Florian Mtey amesema wahitimu hao asilimia kubwa wameshaajiriwa na taasisi mbalimbali ikiwemo hoteli.
"Kikubwa mkafanye kazi kwa kuzingatia uzalendo na maslahi ya taifa katika kuwapokea wageni na kuhakikisha tunatimiza malengo ya kufikisha wageni 5000 milioni ifikapo mwaka 2025," amesema
Dk Mtey amesema idadi ya wanafunzi wanaojiunga na chuo hicho imekuwa ikiongezeka kila mwaka jambo linalowafanya kuendelea kuweka mipango dhabiti ya kusaidia.