Wajackoyah afanikiwa kupiga kura

Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Roots, George Wajackoya akipiga kura

Muktasari:

Baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Roots, George Wajackoya kushindwa kupiga kura asubuhi kutokana na mashine za kieletroniki za kumtambua mpiga kura (Kiems) kushindwa kumtambua, hatimaye majira ya mchana amerudi tena kwenye kituo cha shule ya msingi Indangalasia na kufanikiwa kupiga kura.

Nairobi. Baada ya mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Roots, George Wajackoya kushindwa kupiga kura asubuhi kutokana na mashine za kieletroniki za kumtambua mpiga kura (Kiems) kushindwa kumtambua, hatimaye majira ya mchana amerudi tena kwenye kituo cha shule ya msingi Indangalasia na kufanikiwa kupiga kura.

Wajackoyah aliyekuwa amevaliwa tisheti yenye maandishi ya kusifia bangi, ambayo ni moja ya sera yake amefanikisha zoezi hilo kwa njia mbadala ya kutumia orodha iliyopo kwenye daftari la wapiga kura kama mahakama ilivyotoa amri wiki iliyopita.

Mgombea huyo baada ya Kiems kushindwa kumtambua alirudi kwenye makazi yake kaunti ya Kakamega na picha zake zilisambaa mtandaoni akiwa amepiga magoti kando na kaburi nyumbani kwake.