Wajackoyah ana kwa ana na Kikwete

Wajackoyah ana kwa ana na Kikwete

What you need to know:

Muda mfupi tangu Kiongozi wa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jakaya Kikwete kueleze jinsi alivyoshindwa kukutana na mgombea urais wa Chama cha Roots, George Wajackoyah na kulazimika kuzungumza naye kwa njia ya simu, hatimaye wawili hao wamekutana.

Nairobi. Muda mfupi tangu Kiongozi wa wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022 kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jakaya Kikwete kueleze jinsi alivyoshindwa kukutana na mgombea urais wa Chama cha Roots, George Wajackoyah na kulazimika kuzungumza naye kwa njia ya simu, hatimaye wawili hao wamekutana.

Wawili hao wamekutana na kufanya mazungumzo leo Alhamisi Agosti 11, 2022 jioni ya leo.

Kikwete amesema kuwa kama wasimamizi kutoka EAC walikuwa na wajibu wa kukutana na wagombea wote wa urais, vyombo vya dola na wadau mbalimbali kwa ajili ya kupata hali halisi ya uchaguzi huo lakini kwa bahati mbaya alishindwa kukutana na George Wajackoyah aliyekuwa kijijini kwao.

Baada ya Kikwete kuzungumza hayo wakati akiwasilisha ripoti ya awali ya hali ya uchaguzi nchini humo saa saba baadaye picha na video fupi zilisambaa zikimuonyesha Rais huyo wa awamu ya nne wa Tanzania akizungumza na Wajackoyah kwenye eneo la kuhesabia kura la Bomas jijini Nairobi.

Mgombea huyo wa chama cha Roots aliyetamba na sera ya kuruhusu kilimo na uuzaji wa bangi nchini Kenya mpa saa moja na nusu jioni alikuwa nyuma ya wagombea wawili Ruto na Odinga kwenye idadi ya kura, huku yeye akipata kura 58,900 mpaka muda huo.