Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakulima wa mwani waiangukia Serikali, waiomba kupandisha bei

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Wakulima wa zao la mwani wa Mkoa wa Lindi na Mtwara wameiomba Serikali kuwasaidia katika kupandisha bei zao hilo ili waweze kujiongezea vipato.

Lindi. Wakulima wa zao la mwani wa Mkoa wa Lindi na Mtwara wameiomba Serikali kuwasaidia katika kupandisha bei zao hilo ili waweze kujiongezea vipato.

Pia wamewataka wawekezaji nchini kujitokeza kwa wingi kununua zao hilo kwani limeanza kuongezewa thamani katika matumizi yake.

Mmoja wa wakulima katika kikundi kinacholima zao hilo, Subira Muhibu amesema licha ya kilimo hicho kuwa na fursa kwao lakini kunachangamoto kubwa ya hela ya ununuzi kuwa ndogo.

Amesema zao hilo ni miongoni mwa mazao ambayo yakiongezewa thamani yanaweza kuwainua wakulima hao kupata fedha za kujikimu maisha katika mikoa hiyo.

Muhiba amesema awali kila mwanakikundi katika kikundi chao  alikuwa akiingia baharini na kulima mwenyewe zao hilo ila kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa kamba za kupandia zao hilo ulifanya kuvuna mwani kidogo.

"Baada ya kukaa na kupata mafunzo mbalimbali ikiwemo ya ujasiriamali, ujuzi wa kilimo cha mwani pamoja na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kutokana na zao hilo tuliweza kupata mazao mengi ambapo awali tulikuwa hatupati," amesema Muhiba na kuongeza

”Tulipomaliza mafunzo tuliyopewa na shirika linalopambana na kupiga vita umasikini nchini (Msoapo) tulianza kuhamasishana kujiunga katika vikundi kutokana na utayari wetu wa kuamua kufanya kazi kwa pamoja za kulima mwani na kutengeneza bidhaa zitokanazo na mwani,” amesema

Muhibu amesema wao kama wanawake kupitia zao hilo wanategemea kufanikiwa kwa kukua kiuchumi kwani watakapovuna vizuri na kuuza bidhaa hiyo kwa bei nzuri watapata fedha za kujikimu kimaisha.

Amesema kuwa kwa sasa wanavuna kila mwezi zao hilo kutokana na shirka la Msoapo kuwawezesha vitendea kazi mbalimabali vikiwamo kamba 200 ambapo walikuwa wanavuna kilo 200 hadi 300  za mwani baada ya kupatiwa kamba hizo wanavuna kilo 800 hadi 1000 za zao hilo.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha Juhudi katika Kijiji hicho, Hadija Mohamedi anasema wapo katika hatua ya mwisho ya kufungua kiwanda cha kutengenezea bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao hilo la mwani.

“Naiomba Serikali itusaidie sisi kama wanawake ambao tumedhubutu kujitolea kimaisha katika kujikwamua kiuchumi, tusaidiwe vifaa vya kubebea mwani kutoka baharini kwani tunapata shida mara nyingi kubeba zao hilo kichwani,” amesema Hadija

Amesema soko la zao hilo bado linasuasua kwani wanauza kwa hasara kwa Sh500 kwa kilo moja tofauti na maeneo ya mikoa mingine.

Ofisa Habari wa Shirika la Msoapo, Hamad Hamis amesema shirika lao linalenga kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi na kuwasaidia katika kujikwamua kiuchumi.