Wanafunzi 1, 723 , walimu 49 wanachangia choo kimoja

Wednesday August 04 2021
choopic
By Daniel Makaka.

Sengerema. Wanafunzi 1723 na walimu 49 wa shule ya msingi Sengerema Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wanatumia choo kimoja kutoka na uhaba wa vyoo kwenye shule hiyo.


Mkuu wa shule ya msingi Sengerema Baraka Chitalilo amesema hali hiyo imetokana na shule hiyo kutokuwa na choo Cha walimu na matundu machache ya vyoo vya wanafunzi.


Kutoka na hali hiyo mbunge wa Jimbo Sengerema Hamis Tabasamu ametembelea shule hiyo na kutoa  tofali 2000 na Sh1milioni  kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyoo hivyo.

Advertisement