Wananchi waandamana, wafunga barabara Mkata

Baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Mkata wilayani Handeni wakiwa katika Kituo cha Polisi Mkata wakishikiniza mwenzao aliyekamatwa kuachiwa. Picha na Rajabu Athuman
Muktasari:
Baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Mkata wilayani Handeni wameandamana na kufunga barabara huku wengine wakiwa katika Kituo cha Polisi Mkata wakishikiniza mwenzao aliyekamatwa kuachiwa.
Handeni. Baadhi ya wananchi wa mji mdogo wa Mkata wilayani Handeni wameandamana na kufunga barabara huku wengine wakiwa katika Kituo cha Polisi Mkata wakishikiniza mwenzao aliyekamatwa kuachiwa.
Wananchi hao wakiwamo madereva wa bodaboda ambao wameandamana leo Jumatano Aprili 27, 2022 wamesema kuwa mwenzao ambaye ni dereva wa bodaboda alikamatwa juzi Jumatatu na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe yupo eneo la tukio ili kuongea na wananchi hao.
Endelea kufuatilia Mwananchi kupata taarifa kamili