Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wananchi walia maji kuweka ndoa zao hatarini

Muktasari:

  • Wakazi Kimambi wameiomba Serikali kuwaongezea tanki la maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya binadamu ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu na usiku wa manane kwa ajili ya kutafuta huduma hiyo huku wakiwaacha waume zao kitandani.

Liwale. Wakazi zaidi ya 3,000 wanaoishi katika kijiji na Kata ya Kimambi wilayani Liwale mkoani hapa, wanaiomba Serikali kuwaongezea tanki lingine la maji, kwani lililopo halikidhi mahitaji ya wakazi hao na maji yaliyopo sasa ni ya chumvi ambayo hayafai kwa matumizi ya kunywa.

Wakizungumza na Mwananchi Digital wakazi hao leo Ijumaa Oktoba 20, 2023 wamesema kuwa wanalazimika kutembea zaidi ya kilometa 5 usiku wa manane kufuata maji na kuweka ndoa zao hatarini pamoja na uhai wao.

Wamesema kuwa maji wanayotumia sasa hivi wanapikia na kufulia kwa shida kutokana na maji safi yapo mbali na wanayapata umbali zaidi ya kilometa 5 na maji hayo ni ya chemchemi.

Hawa Shaweji ambaye ni Mkazi wa Kata ya Kimambi, amesema kuwa wanatembea umbali mrefu zaidi ya kilometa 5 kufuata ya maji ya chemichemi katika eneo la Njengani na amesema kuwa wakati wakwenda kuchota maji wanakutana na wanyama wakali kama tembo ambao wanahatarisha maisha yao.

 "Natoka nyumbani saa tisa usiku kwenda kuchota maji, kurudi hadi saa 8 mchana hivi mwanaume gani anaweza kuvumilia hali hiyo, tunagombana na wanaume zetu kila wakati, mimi niiombe Serikali itupatie tanki la maji lililokubwa na lenye maji salama kama yale ya chemi chemi ilikutuondolea adha hii,” amesema Hawa.

Mkazi mwingine Mussa Litago amesema kuwa maji wanayoyapata katika chemchemi hiyo ni ya foleni, amesema kuwa wanaweza kwenda asubuhi na kurudi jioni, wanakwenda kwa umbali mrefu kwa kuwa wanahitaji maji ya kunywa ambayo hayana chumvi.

 "Tunakwenda umbali mrefu kwa kuwa maji ni baridi yanatusaidia kwa kunywa, maji yaliyopo sasa ambayo tumewekewa tanki dogo ni ya chumvi, haya maji ya chumvi tunayatumia kwa ajili ya kufulia kupikia na kuoshea vyombo. Sisi wananchi wa Kimambi tunateseka na maji, Serikali itusaidie kutuletea maji safi na salama," amesema Litago.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) wilayani Liwale, Mhandisi Joseph Mbio amesema kuwa katika kata hiyo wanacho chanzo kimoja ambacho ni kisima na wamewekewa tanki,   changamoto iliyopo  maji  wanayotumia kwa sasa ni ya  chumvi, amesema kuwa wameshaongea na watu wa Bonde la Mto  Ruvuma kwa ajili ya kuja  kufanya utafiti ili kuweza kuchimba kisima kingine iliwapate maji safi, ambayo siyo ya chumvi.

"Ruwasa tumeshaongea na watu wa Mto Ruvuma kuja kufanya utafiti ili kuweza kuchimba kisima kingine ili wananchi waweze kupata maji yaliyosafi zaidi ambayo yatakuwa hayana chumvi," amesema Mbio.