Wananchi waonywa tabia ya kutoboa bomba la maji

Jamii ya wafugaji Kijiji vha Ndinyika wilayani Siha mkoani Kilimanjaro, wakiwa kwenye hitimisho la wiki ya maji katika kijiji hicho

DC aonya wananchi kuhujumu miundombinu ya majiSiha. Mradi wa Maji unaojengwa na mkandarasi kutoka Kampuni ya Poshi Alliance Limited ambao utavinufaisha Vijiji vya Ndinyika, Lekrimuni, Kandashi na Mawasiliano Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro unatarajia kukamilika Aprili 15 mwaka huu.

Kondo Juma Makamu Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) akitoa taarifa upanuzi wa skimu ya Gararagua kutoka Tantred Farm kwende kwenda kwenye hivyo wakati wa kilele cha Wiki ya Maji maadhimisho yaliyofanyika Kijiji cha Ndinyika Wilayani humo.

Katika taarifa yake aliyoitoa  kwa mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Timbuka amesema mradi huo unaogharimu zaidi ya Sh700 milioni lengo ni kuongeza wingi wa maji katika eneo hilo na kunufaisha wananchi wapatao 11.049. Mradi huu unatekelezwa wilayani Hai na Siha.

Amesema mradi huo unafanyika kupitia fedha za IMF (COVID) na Mfuko wa Maji wa Taifa, mradi huo ulianza kutelekezwa Decemba 12, 2021 unatarajia kukamilika April 15 mwaka huu. Mradi umefikia asilimia 98 ya utekelezaji.

Pia amesema Ruwasa wilayani humo inaendelea kufanya utanuzi wa mtandao wa bomba kwa maeneo ambayo mradi haijafika na kuongeza vituo vitatu vya kuchota maji kupitia fedha za makusanyo ya ankra ya maji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Magadini Makiwaru, Monika Kimbi ametaka mradi huo kumalizika kwa wakati ili watu wapate maji kwa wingi na kuleta maendeleo.

Gres Mollel na Neema Lukumay wakazi wa maeneo hayo wamesema wamekuwa wakitembea umbali wa kilometa 15 kufuata maji, hivyo kukamilika kwa mradi huo kutawaondolea usumbufu huo na kumpongeza Mama Samia Suluhuu Hassan kwa kuwaletea maji karibu.

Shedrack Mosha kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Timbuka wakati wa kuweka jiwe la msigi, amewataka wananchi wa maeneo hayo kulinda miundombinu ya maji.

"Ili uweze kukaa kwa muda mrefu mradi huu, msifanye hujuma wa kutoboa mabomba ili mpate maji ya wanyama huo ni ubinafsi ilindeni, ikiharibi maji mnakosa nyie sio sisi," amesema Mosha.