Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanaouza vitambulisho vya Nida kukamatwa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas (kushoto) akimkabidhi Sada Said mfano wa kitambulisho cha uraia (NIDA) katika hafla iliyofanyika ufukoni Manispaa ya Mtwara Mikindani. Picha na Florence Sanawa

Muktasari:

  • Zaidi ya vitambulisho 300,000 vya uraia (Nida) vimegawiwa mkoani hapa kwa wananchi hatua ambayo itapunguza kero ya usahaulifu wa namba ambayo ni changamoto kubwa kwa wananchi. 

Mtwara. Zaidi ya vitambulisho 300,000 vya uraia (Nida) vimegawiwa mkoani hapa kwa wananchi hatua ambayo itapunguza kero ya usahaulifu wa namba ambazo zimekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi wanapohitaji huduma mbalimbali za kijamii na Serikali.

Asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa wakitumia namba pekee za Nida huku wakiwa hawana vitambulisho hali ambayo imekuwa ikipelekea kusahau namba hizo.

Akizindua zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho 300,000 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanal Ahmed Abbas amesema kuwa ugawaji wa vitambulisho hivyo ni zoezi endelevu.

Amesema wote waliosajiliwa watapatiwa na hata ambao hawajasajiriwa wanapaswa  kujisajiri  ili kuweza kupata huduma mbalimbali za kijamii.

“Hivi vitambulisho vilishawahi kutolewa awali lakini kwa mkoa mzima vilitoka zaidi ya 200,000, idadi ya leo sio ndogo na vinatolewa bure kwa wananchi wote. Niwaaagize watendaji kuhakikisha kuwa wanazingatia sheria na kanuni ili viweze kuwafikia wananchi wote siyo busara kuona vitambulisho hivyo vikiwa ofisini tu,” amesema Kanal Abbas.

“Gaweni bure vitambulisho hivi acheni kukaa navyo na kusababisha kutengeneza mazingira ya rushwa na masivumilie hujuma za wananachi juu ya vitambulisho hivyo chukueni hatua” amesema Kanal Abbas.

Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Shadida Ndile amesema kuwa ujio wa vitambulisho hivyo utapunguza kero walizokuwa wanakutana nazo wananchi.

“Vitambulisho vya Taifa vilikuwa kero kwa wakazi wa Mtwara na tunatambua umuhimu wake ndiyo maana wataanza watu walikuwa wakipanga foleni ndefu ili kuweza kupata vitambulisho hivyo,” amesema Ndile.

Mkuu wa Wilaya ya Newala, Alhaj Kundya Mwangi amesema kuwa vitambulisho hivyo ni muhimu kwa kuwa Newala ipo mpakani, hii itatusaidia na kupunguza mitihani tuliyokuwa tunakutana nayo.

“Ukosefu wa vitambulisho ulikuwa unatupa wakati mgumu kwakuwa ulikuwa huwezi kutofatisha kati ya mgeni na mwenyeji hasa katika wilaya yetu ambayo iko karibu na mpaka,” amesema.