Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne matatani  wakidaiwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Sehemu ya punda 46 waliokamatwa wakisafirishwa nje ya nchi kinyume na utaratibu, wilayani Longido mkoani  Arusha jana, ambapo watuhumiwa wanne wanaodaiwa kusafirisha wanyama hao wakishikiliwa kwa hatua zaidi.

Muktasari:

  • Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kuzuia wizi wa mifugo nchini, SACP Simon Pasua amesema tayari Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilishatoa katazo la kusafirisha punda na mazao yake kutokana na kupungua kwa idadi ya wanyama hao nchini.

Arusha. Jeshi la Polisi Kikosi cha Kupambana na Kuzuia wizi wa Mifugo kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, linawashikilia watuhumiwa wanne wakidaiwa kusafirisha nje ya nchi punda 46 kinyume na taratibu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi Mei 25, 2024 na  Kamanda wa kikosi hicho nchini, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Simon Pasua watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa wanasafirisha punda hao kinyume na utaratibu.

Amesema kuwa watuhumiwa hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huku majinayao yakihifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

“Upelelezi utakapokamilika watuhumiwa wote watafikishwa katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili,”imeeleza sehemu ya taarifa hiyo

Kamanda Pasua amesema tayari Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilishatoa maelekezo juu ya katazo la kusafirisha punda na mazao yake kutokana na kupungua kwa idadi ya punda nchini.

"Kwa kushirikiana na maaskari wa doria tumekamata punda 46 wakiwa wanasafirishwa nje ya nchi kinyume na utaratibu, watuhumiwa wanne wanashukiliwa na uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.”

"Tutaendelea kuwakamata wote wanaokiuka taratibu za kusafirisha punda na mazao yake kwenda nje ya nchi. Punda wamekatazwa kusafirishwa nje ya nchi kutokana na idadi kuwa ndogo hapa nchini,"amesema.

Kamanda huyo aliwataka wananchi kuzingatia sheria na kuhakikisha wanaposafirisha wanyama au mazao yake wana vibali maalumu vinavyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.