Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanne TPA wafikishwa mahakamani

Wanne PTA wafikishwa mahakamani

Muktasari:

  • Watu watano wakiwemo wanyakazi wanne wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) wa Kitengo cha Uhasibu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuingiza data za uongo kwenye mfumo wa malipo.

Dar es Salaam. Watu watano wakiwamo wanyakazi wanne wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA) wa Kitengo cha Uhasibu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kuingiza data za uongo kwenye mfumo wa malipo na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh694 milioni.

 Washtakiwa hao ni Steven Swai(35),Philip Sengele(43),Ally Mwinjimvua(49) na Laurent Filbert(35) wote ni wahasibu kutoka TPA pamoja na Mohamed Swalehe(22) ambaye alikuwa kibarua wa mamlaka hiyo.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Romuli Mbuya,Wakilinwa serikali Mwandamizi,Grace Mwanga alidai tarehe tofauti  Kati ya Julai Mosi ,2019 na Novemba 30,2021 katika maeneo ya Mamlaka ya Bandari washtakiwa hao Kwa pamoja waliingiza data kwenye mfumo jambo ambalo wameisababishia serikali hasara ya Sh 694,072,463.90

Mwanga alidai upelelezi bado unaendelea hivyo aliiomba Mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo Wakili wa utetezi,Abriat Kivela aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa Swai alilazwa kwa siku tano katika hospitali ya Agha Khan chini ya uangalizi wa serikali na anaendelea na dozi hivyo anapoenda mahabusilu awe chini ya uangalizi

Hakimu Mbuya alisema hilo ni shauri la uhujumu uchumi washtakiwa hawana haki ya kupata dhamana. Shauri Hilo limeahirishwa Hadi Desemba 29,2021 Kwa ajili ya kutajwa