Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wataka mtoto wa kike apewe fursa kutoa maoni

Muktasari:

  • Kila mwaka ifikapo, Oktoba 11, dunia huadhimisha siku ya kimataifa ya Mtoto wa Kike (IDGC), ili kusherehekea mafanikio na uwezo wa wasichana, kutambua haki zao na kubaini changamoto za kipekee wanazokutana nazo ulimwenguni.

Dar es Salaam. Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike (IDGC), Oktoba 11 mwaka huu, jamii imetakiwa kuwapa fursa mabinti ya kutoa maoni yao katika masuala yanayowahusu.

Wito huo umetolewa leo Septemba 11, 2024 na baadhi ya mabinti vinara wakati wakisoma tamko lao katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Pia wamewataka wasichana walioko shuleni kujitokeza kugombea fursa mbalimbali za uongozi wa wanafunzi wenzao zinapojitokeza.

Mmoja wa wasichana viongozi kutoka Shule ya Msingi Boma, Esther Abduely amesema utafiti unaonyesha kuwa asilimia 44.4 ya wanafunzi wa sekondari hawaelewi maana yademokrasia, huku asilimia 85.5 hawajawahi kushiriki, kushirikishwa kati ka vikao rasmi vya shule vinavyofanya uamuzi.

Amesema asilimia 68.9 ya wanafunzi hawajawahi kugombea au kuonesha nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ngazi ya shule, huku asilimia 44 hawashiriki katika chaguzi za uongozi wa wanafunzi.

Wamesema katika ngazi ya jamii, mtoto wa kiume anashirikishwa na kutoa mawazo yake kuhusu masuala mbalimbali ya kimaendeo nyumbani, ikiwa mtoto wa kike hapewi nafasi hiyo au anapaswa kuwa msikilizaji tu na mtekelezaji wa maamuzi yanayofanyika.

Kwa upande wake Angle Mohammed amesema hiyo ndiyo sababu maadhimisho ya mwaka huu kupitia ajenda ya ‘Masichana 2024’ inayotarajia kukutanisha wasichana takribani 200 jijini Dodoma kujadili mada za wasichana na uongozi kati ka karne hii ya kidigitali, changamoto na fursa zinazotokana na nafasi mbalimbali za uongozi na jinsi fursa za uongozi zinavyoweza kutumika kuwainua wasichana kati ka sekta ya elimu pamoja na Afya, na kijinsia.
Amesema ajenda hiyo inalenga kufungua milango ya fursa kwa wasichana kujifunza, kujieleza na kusimamia mabadiliko chanya katika jamii zao.

"Katika kuadhimisha siku hii muhimu mwaka huu wadau wa haki za wasichana kutoka mashirika saba ikiwemo Msichana Initiative, TAI, GLAMI, Flaviana Matata, C-Sema ,Young Mothers Foundation na Wite sawa wameshirikiana katika kuandaa maadhimisho haya yaliyobeba kauli mbiu ya "wasichana na uongozi, kutumia fursa ya teknolojia za kidigitali," amesema.

Amesema kabla ya kilele hicho wataweza kufanya matukio mbalimbali katika mikoa ya Arusha, Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Dodoma, Mbeya pamoja na Zanzibar, ambapo yatuwakutanisha na wasichana wengine ili kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusu kaulimbiu ya mwaka huu.

Naye Mratibu wa Programu kutoka Taasisi ya Flaviana Matata, Brian Terry amesema kila mmoja anajukumu la kuhakikisha kuwa anajenga mazingira ambayo yatampa mtoto wa kike nafasi ya kustawi, kujifunza, na kutumia vipaji vyake kikamilifu.

Amesema katika kusherekea maadhimisho hayo wataweza kuwapa elimu ya Uongozi na Tekinologia wasichana hao na kukusanya maoni yao kwa lengo la kutomuacha mtu nyuma na kuhakikisha sauti za mabinti zinasikika.