Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watakiwa kuzalisha chakula kuondokana na udumavu

Muktasari:

  • Ili kuondoka na udumavu, wakulima katika mikoa ya Lindi na Mtwara wameshauriwa kutosahau uzalishaji wa chakula kwa kutumia mbegu za asili na ambazo zimefanyiwa utafiti, jambo ambalo pia litawezesha mikoa hiyo kuwa kuwa chakula cha kutosha.

Masasi. Wakulima katika mikoa ya Lindi na Mtwara wameshauriwa kuzalisha chakula kwa kutumia mbegu za asili na ambazo zimefanyiwa utafiti, jambo ambalo pia litawezesha mikoa hiyo kuwa kuwa chakula kutosha lakini pia kuondokana na udumavu kwa watoto.

Mratibu wa mtandao wa Bioanuwai Tanzania (Tabio), Abdala Mkindi ameyasema hayo wakati wa mafunzo yaliyofanyika jana kwa wakulima ambayo yamejikita katika matumizi ya mbegu za asili na zile zilizofanyiwa utafiti, huku akihimiza uzalishaji wa chakula.

"Lengo ya haya mafunzo, ni kuwajengea uwezo wakulima wetu katika kulima kilimo cha chakula na mboga mboga, kwani kwa sasa wengi wa wakulima wameachana na kilimo cha mbogamboga, jambo ambalo limesababisha mikoa ya kusini kuwa na udumavu kwa watoto," amesema Mkindi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, Masumbuko Mtesigwa ameonyesha kuridhishwa na namna NGOs zinavyoshirikiana na wakulima, zikiwafundisha juu ya matumizi bora ya ardh, utunzaji wa mazingira, na kilimo bora.

"Serikali inasisitiza wakulima wetu wasilime kilimo cha biashara peke yake, pia wajitahidi kulima mazao ya chakula ili kuweza kujitosheleza kwa chakula na pia watoto wetu waweze kuwa na lishe bora," amesema.

Mshauri wa Kilimo kutoka Mkoa walindi Hadija Bakili amesema mafunzo yaliyotolewa kwa wakulima, yatasaidia kuongeza tija katika mazao ya chakula na mboga mboga, hivyo, amewataka wakulima kuzalisha kwa wingi ili Lindi na Mtwara ziweze kujitosheleza kwa chakula

Mmoja wa wakulima wanufaika na elimu hiyo, Sara Malidadi, amesema kuwa mafunzo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa kuzalisha mazao ya chakula zaidi, ilikuweza kujitosheleza kwa chakula, na kufanya watoto wao kupata lishe bora kwa kutumia mbegu za asili.

Imeelezwa kuwa mradi huo wa mafunzo kwa wakulima ni wa miaka miwili na kwamba utazinufaisha kaya 1400, katika mikoa ya Mtwara na Lindi ambapo uzalishaji wa chakula unaokana kelagalega.


Mwishoo....