Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watatu wakamatwa wakituhumiwa kuiba nyaya za umeme

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP-Mtaki Kurwijila akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichan).

Muktasari:

  • Watu watatu wamekamatwa wilayani Masasi mkoani Mtwara kwa tuhuma za kuiba nyaya za umeme mafungu saba na kutoroka nazo wakiwa na pikipiki moja ndani ya gari walilokuwa wakilitumia.

Mtwara. Jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara limewakamata watu watatu kwa tuhuma za kuiba nyaya za umeme mafungu saba waliyokuwa wakiyasafirisha kwa kutumia gari aina ya canter.

Akizungumzia tukio hilo Februari 20, 2024 ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Mtaki Kurwijila amesema kuwa walipokea taarifa ya uwepo wa wizi wa nyaya za umeme ambapo Jeshi la Polisi Wilaya ya Masasi walianza ufuatiliaji na kufanikiwa kuwakamata watuhimiwa hao.

Kamanda amewataja waliokamatwa kuwa ni Hamidu Nassoro Ngonyani (33) Faridi Mohamed (24) na James Mathayo (28) ambapo walikamatwa wakiwa wanasafirisha nyaya hizo.

Amesema kuwa pamoja na kukamata watuhumiwa hao pia walikutwa wakisafirisha pikipiki moja aina ya TVs yenye namba MC713 BCH kwa kutumia gari aina ya Canter yenye namba za usajili T596DYD ambapo vyote wa jumla mpaka sasa thamani yake  haijafahamika.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja kutoka Shirika la Umeme (Tanesco) Mkoa wa Mtwara, Jumanne Nkunguu amesema kuwa kuibiwa kwa nyaya hizo ni kurudisha nyuma jitihada za Serikali za kusogeza umeme kwa wananchi vijijini.

Amesema kuwa wizi wa vifaa kwenye miradi inasababisha isikamilike kwa  wakati hali ambayo inakatisha tamaa wananchi na kuwatia hofu wakandarasi.

“Mkandarasi akipewa kazi ina maana anapewa ukubwa wa eneo na pia muda wa kuanza na kumaliza, endapo ataibiwa vifaa kama hizo nyaya hawezi kukamilisha kama ilivyokusudiwa.”

“Hata ukiangalia wananchi ambao hawana umeme na walitegemea kupata haraka, lakini wanakosa kwa wakati kutokana na kuwepo kwa watu wasio  waaminifu na wanaokwamisha kazi za wakandarasi wetu,” amesema Nkunguu.