Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri apigia debe Tanzania ya viwanda mashuleni

Muktasari:

Pia amewakumbusha  watanzania wasikimbilie kwenye uanzishaji wa viwanda vikubwa bali waanze na vidogo.

Bukoba. Kama alivyowahi kunukuliwa kwamba yeye ni mpiga debe wa Tanzania ya Viwanda,leo Waziri Charles Mwijage amehamishia debe hilo kwenye shule za sekondari akisema wanafunzi waandaliwe kuchukua jukumu mbeleni kwa kuwa viwanda vinavyojengwa sasa ni vile vya kipindi cha mpito.

 

Akihutubia katika mahafali ya kidato cha sita kwa shule za sekondari Kaizirege na Kemebos, leo Mei 19, Waziri Mwijage,amesema viwanda vya kudumu vitajengwa na wanafunzi wanaoandaliwa vizuri katika masomo ya sayansi.

 

Amesema kuwa wazazi na wanafunzi wanatakiwa kusoma upepo unapoelekea ambao unawahitaji wanafunzi wa masomi ya sayansi kwa ajili ya kuchukua jukumu la.kujenga uchumi wa viwanda.

 

Pia amewakumbusha wazazi na watu wenye mitaji wasikimbilie kwenye uanzishaji wa viwanda vikubwa bali waanze na viwanda vidogo na baadaye waende hatua kwa hatua hadi viwanda vikubwa.

 

 

Waziri Charles Mwijage ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kudato cha sita shule ya Sekondari Kaizirege na ya Kemebos ambapo jumla ya wanafunzi 180 wamehitimu.