Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waziri Ummy aonya wanaotiririsha maji taka

Muktasari:

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha hatua kali zinachukuliwa kwa wananchi wanaotiririsha maji taka ya vyoo nyakati za mvua.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya nchini Tanzania, Ummy Mwalimu ametangaza kibano kipya kwa wananchi wanaotirisha maji taka barabarani nyakati za mvua, akizitaka halmashauri zote nchi kuhakikisha sheria zao zinakuwa kali kudhiti tabia hiyo.

 Amesema ni vyema halmashauri zote nchini kuhakikisha faini wanazolipishwa watu wenye tabia hizo ni kubwa kuliko gharama ya kukodi gari kuchukua maji taka hayo majumbani.

Waziri Ummy aliyasema hayo leo Jumatatu Agosti 29, 2022 kwenye semina ya kujengeana uwezo kuhusu namna ya kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ukizishirikisha nchi tano.

Katika semina hiyo ya siku tano kuanzia  Agosti 29 hadi Septemba 2, 2022 wawakilishi kutoka nchi tano wanashiriki wakitokea  Angola, Zambia, Malawi, Msumbiji na Tanzania.

Waziri Ummy amesema, tabia ya baadhi ya wananchi hususani wa mijini nyakati za mvua kufungulia maji taka barabarani ni hatari kwani maji hayo ni chanzo cha kipindupindu akizitaka halmashauri zote nchi kuwachukulia hatua wahusika.

"Ni wakati sasa wa hizi halmashauri kutekeleza sheria ndogondogo walizonazo,” amesema


“Kwa kipindi cha mwaka huu, tayari mikoa mitatu ya Rukwa, Kigoma na Katavi zimeripoti visa 519 na vifo 11 vitokanavyo na ugonjwa wa kipindupindu.”

“Niagize wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kote nchini hususan mikoa hii iliyoripoti kipindupindu kuhakikisha wanakuwa na mkakati wa pamoja na taasisi zinginezo kudhibiti kipindupindu kwenye maeneo yao,"alisema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema, katika kudhibiti ugonjwa wa kipindupindu nchini serikali itahakikisha maeneo yanayoripotiwa visa vya ugonjwa huo maji yanapatikana.

Naye Kaimu Mwakilishi Mkaazi wa WHO, Dk Yoti Zablon amesema, ugonjwa wa kipindupindu katika nchi za Afrika ni asilimia 20 lakini jambo la kustaajabisha pamoja na idadi ya ndogo ya watu wanaougundua Afrika inachangia asilimia 80 ya vifo vinavyotokana na kipindupindu duniani.

Changamoto kubwa aliyoitaja ni wagonjwa kutogundulika kwa wakati na matibabu kwa wagonjwa kutopatikana kwa muda unaohotajika.