Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Udhibiti viuatilifu wapaisha kilimo cha mbogamboga

Tanzania imefanya jitihada mbalimbali za kuwezesha wakulima wadogo na kuvutia uwekezaji nchini, kwa kuweka mazingira wezeshi ya biashara kupitia mageuzi ya kimkakati, ili kuhakikisha vikwazo vya udhibiti vinaondolewa.

Mushobozi Baitani ni mtaalamu wa kulinda afya ya mimea na kupambana na wadudu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula (FAO) ambalo pia limeshiriki katika mpango wa kuiwezesha Tanzania kufanya maboresho ya mifumo na sheria ili kuleta tija katika sekta ya kilimo.

Anasema katika utafiti wao kabla ya kufanya maboresho hayo miaka michache iliyopita, walibaini kuwa soko la parachichi kutoka Tanzania katika nchi za India, China na Afrika Kusini lilikosa thamani kwa sababu ya kutishiwa na wadudu waharibifu wanaoitwa ‘Quarantine Pests’ ambao waliathiri ubora wa matunda hayo.

Hivyo, kupitia Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Afya ya Mimea (IPPC), ambao Tanzania pia ulisaini, zao hilo lilizuiwa katika soko la kimataifa.

Lakini changamoto hiyo ilifanyiwa kazi kwa sababu kuu mbili, kwanza kulinda soko na pili ilikuwa kwa ajili ya matokeo ya utafiti uliofanywa na Umoja wa Ulaya (EU) ambayo imefadhili mradi huo kwa kupitia wadau mbalimbali wakiwemo FAO na International Finance Corporation (IFC) ambao ni sehemu ya Benki ya Dunia.

‘’Utaratibu rahisi pia wa usajili wa kemikali ya viuatilifu ulianzishwa ili kuwa na usafirishaji safi wa mazao nje ya nchi,’’ anasema.

Kwa hiyo, anasema Tanzania ilihitaji mfumo imara wa kitaasisi ili kufanyia kazi masuala ya viuatilifu, sababu iliyochangia kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kusimamia Afya ya Mimea na Kudhibiti Viuatilifu hapa nchini (TPHPA) iliyoanzishwa mwaka 2020.

Kupitia maabara zake ndogo zilizopo nchini, anasema TPHPA ikapewa ithibati ya kuangalia mabaki ya wadudu katika mazao kwa gharama nafuu kabla ya mazao hayo kupelekewa nje ya nchi kwa gharama nafuu zaidi tofauti na hapo awali.

‘’ Hivi sasa baada ya maboresho yanayoendelea kufanyika, mauzo ya nje yanatarajiwa kuongezeka kwa kasi kutoka asilimia 30 hadi 60 baada ya kumalizika kwa mradi wa afya ya mimea,m ‘’anasema.

Farida Mfinanga ambaye ni mkulima na muuzaji wa pembejo mkoani arusha anasema kuanzishwa kwa TPHPA kunafungua ukurasa mpya wa usafirishaji na usimamizi wa viuatilifu hapa nchini na kuwapa faraja wakulima na uhakikia wa kupambana na wadudu waharibifu iii wavune mazao mengi.

Fursa kilimo cha mbogamboga

Shridhar Chaudhary, ni mwekezaji anayesafirisha mazao ya mbogamboga nje ya nchi.

Anasema kuwa amefurahishwa kuja kuwekeza katika sekta ya kilimo cha mbogamboga Tanzania kwa sababu ya kile anachosema, mazingira mazuri yanayochochewa na mageuzi yanayoendelea.

” Tanzania ni nchi nzuri, yenye ardhi nzuri yenye rutuba. Nimeanza kuwekeza Tanzania tangu Oktoba mwaka jana, nikitokea Ghana nilipokuwa nafanya biashara za mahindi kwa kuwekeza zaidi ya ekari 3,000. Na tangu nilipokuja, nimekuwa nikifanya biashara ya kupeleka mazao Ulaya kwa kusafirisha wastani wa tani 60-70 kwa wiki,” anasema.

Anachozingatia zaidi ni kwamba mazao yake yanafika soko la Ulaya kwa urahisi yakiwa bado ’freshi’ .

Anasema kufanya kazi kwake kumekuwa rahisi kupitia mfumo rafiki unaosimamia ufanyakazi kazi wa biashara kimtandao (ATMIS),.

Anasema Chama cha Kilimo cha mazao ya Bustani Tanzania (TAHA) kimemuunganisha na wakulima wachapakazi wanaomsaidia kuzalisha mazao bora kama vile pilipili za mwendokasi pamoja na mazao mengine ya biashara ya muda mfupi.

Solomon Baregu ni ofisa anayeshiriki katika kusimamia mageuzi ya mifumo wezeshi ya ufanyaji biashara katika Shirika la Kimataifa la Fedha (IFC). IFC hasa inafanya kazi katika sekta ya kilimo cha bustani ambapo miongoni mwa changamoto ilizoziona, ni katika mchakato wa uingizaji na usajili wa viuatilifu na kemikali mbalimbali za kilimo nchini Tanzania.

Ikiwa ni sehemu ya Benki ya Dunia, IFC ndiyo taasisi kubwa zaidi ya maendeleo duniani inayojikita katika kusaidia sekta binafsi katika nchi zinazoendelea, ikiwamo Tanzania.

Inatoa huduma za uwekezaji, ushauri na usimamizi wa mali ili kuhimiza maendeleo ya sekta binafsi katika nchi zilizoendelea kidogo.

Baregu anasema tangu mwaka 2017, wamefanya utafiti wa aina mbalimbali wa utambuzi, ambazo zimekuwa msingi wa kufanya mageuzi hayo.

Anasema utafiti huo ulitoa takwimu za msingi ili kuelewa changamoto zilizoibuliwa na wadau, ambao walilalamikia sera na sheria zinazoonekana kukinzana katika ngazi ya serikali kuu na serikali za mitaa zinazohusiana na maeneo kadhaa kama kodi, ushuru na leseni.

Anasema mwaka 2018, waliona kuwa sekta hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto kadhaa na maeneo ambayo yalilenga kufanyiwa mageuzi ni pamoja na mchakato wa uingizaji na usajili wa viuatilifu na kemikali mbalimbali za kilimo nchini Tanzania.

Sababu hiyo iliifanya IFC kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali kufanya mapitio ya taasisi mbili, Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Tropiki (TPRI) na ile ya Huduma za Afya ya Mimea (PHS).

Ikaonekana ipo haya ya kuwa na taasisi moja yenye nguvu na ndipo TPHPA ikaanzishwa mwaka 2020, huku mikakati ya kuiwezesha kimifumo na kivifaa kwenye maabara zikiwemo zile za kwenye mipaka ikiendelea .

Anasema baada ya hatua hiyo, changamoto zote ambazo wakulima walikuwa wakikabiliana nazo katika eneo la kilimo, sasa zitakuwa historia.