Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanamke anayempamba mchekeshaji Joti

Muktasari:

  • Hata hivyo, kufanya kwake vizuri Joti ukilinganisha na wasanii wengine ni kutokana na namna ambavyo amekuwa mtu wa kubadilika badilika, kwani kuna wakati anakuwa mtoto, dada, mama, babu au kijana nafasi ambazo zote hajawahi kuwaangusha mashabiki wake.

Joti ni kati ya waigizaji wa vichekesho wanaofanya vizuri katika tasnia hiyo, huku moja ya sifa ni kuweza kucheza nafasi zote na kuwateka watazamaji.

Hata hivyo, kufanya kwake vizuri Joti ukilinganisha na wasanii wengine ni kutokana na namna ambavyo amekuwa mtu wa kubadilika badilika, kwani kuna wakati anakuwa mtoto, dada, mama, babu au kijana nafasi ambazo zote hajawahi kuwaangusha mashabiki wake.

Katika nafasi hiyo huwa anajibadilisha kwa kujipamba kama mwanamke ikiwemo kubandika hadi kope, kupaka poda, wanja na kuvaa nywele za bandia na mapambo mbalimbali zikiwemo hereni, mikufu na bangili.

Mtu anayeyafanya hayo si mwingine, bali ni Faudhia Gingi, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Alivyokutana na Joti

Faudhia anasema anakumbuka miaka mitatu iliyopita akiwa saluni kwake maeneo ya Kinondoni, rafiki yake alimuita waende studio ambapo Joti huwa anatengenezea kazi zake.

Pamoja na awali kutojua anapelekwa wapi, Faudhia anasema alipofika huko alimkuta Joti akiwa amevaa gauni, jambo ambalo lilimshtua.

Hata hivyo, Joti alimuondoa wasiwasi na kumwambia asiogope na kisha kuchukua kioo, kujiangalia na kumuuliza kama anaweza kumbadilisha na kuwa na muonekano wa mwanamke.

“Aliponiuliza swali hilo kama naweza kumbadilisha na kuonekana mwanamke, nilijikuta tu namjibu kwa kujiamini kuwa naweza lakini wakati huo najiuliza hivi kweli nitaweza kumbadili mwanaume kuwa kama mwanamke,” anasema Faudhia.

“Nashukuru baada ya kumaliza kazi yangu na alipojiangalia aliridhika na nilichomfanyia suala ambalo lilizidi kunipa moyo kuendelea kufanya naye kazi.

“Siku nyingine tena aliniambia kuwa anataka abadilishwe na kuwa na muonekano wa babu na hii tuliifanya wakati akiandaa tangazo la maziwa ya Dar Fresh, na baada ya kunikubali kuanzia hapo nikawa ndio mpambaji wake hadi leo,” anasema.

Changamoto anazozipitia

Tofauti na kuwapamba wanawake, Faudhia anasema kwa mwanaume kwa kawaida vifaa vya mapambo hutumika vingi kwani mpaka ndevu zisionekanae sio jambo dogo. Pia, inapofika wakati wa kubandika kope, anasema Joti hatutilii kama ilivyo wanawake na hii yote ni kutokana na kuwa mtu wa kupenda kuongea wakati wote.

“Unajua Joti ni mtu anayependa kuongea na kuchekesha, hivyo hata kama mpo katika kupambana kuna wakati inabidi umsubiri amalize na nyie mmalize kucheka ndio muendelee,”anasema.

Jingine anasema huwa anamuonea huruma anapolalamikia ndevu zake anapozikata ili kumpamba, kwa kuwa kuna nafasi nyingine akicheza lazima atoe ndevu ili vipodozi vikae vizuri.

Katika urembo kuna watu ambao huwachukia hasa pale wanapopaka vipodozi mbalimbali, lakini kwa Joti haijawahi kumtokea hata kutokwa na kipele, na hii Faudhia anasema imechangiwa na yeye kutumia vipodozi halisi.

Kama haitoshi anasema hata wakati wa kuvitoa hufuata taratibu zote katika utoaji, tofauti na wengine hufika hatua hata ya kulala navyo.

mpaka asubuhi jambo ambalo sio sahihi.

Wanapata wapi vifaa

Kuhusu mahali wanapopata vifaa vya kupambia, Faudhia anasema ni moja ya vitu ambavyo vipo katika dokezo la kutengeneza kazi za Joti.

Hivyo kila inapotokea anahitajika kupiga picha kwa ajili ya kazi fulani, ujue kuna bajeti ya kuanzia nguo anazovaa hadi vipodozi na kuongeza kuwa anashukuru hawajawahi kudhulumiana hata siku moja tangu walipoanza kazi.