Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pendeza na mtindo mpya wa ‘High Low’

Muktasari:

Hii ni aina la vazi, ambalo limekuwa maarufu hasa kwa wasichana wengi mjini, kutokana na ubora unaotokana mshono wa nguo hizo.

KWENDA na wakati  ni jambo linalopendwa na wanawake wengi kwa kuwa humfanya mwanamke kuonekana wa kisasa na kuzidi kuvutia.

Suala hilo huambatana na uvaaji mzuri wa mavazi yaliyo nadhifu na yenye kuvutia machoni kwa jamii inayokutazama.

Ili mwanamke uonekane  wa kisasa, lazima ujitahidi kwenda na wakati kwa kuvaa nguo zilizo katika chati.

Kama ni mfuatiliaji mzuri wa masuala ya mavazi hautakuwa mgeni na mtindo wa nguo maarufu kama ‘High –Low’.
Hii ni aina la vazi, ambalo limekuwa maarufu hasa kwa wasichana wengi mjini, kutokana na ubora unaotokana mshono wa nguo hizo.
‘High Low’ ni aina ya nguo, ambayo mara nyingi upande mmoja huwa fupi na mwingine huwa mrefu.

Mara nyingi upande wa mbele huwa ni mfupi na nyuma huwa mrefu, ndiyo maana wakaiita ‘high –low’.

Aina hiyo ya nguo, ipo katika mitindo mingi ikiwamo sketi, mashati pamoja na magauni.
Wasichana wengi hupendelea kuvaa shati  za mtindo huo, ambazo mbele huwa fupi na nyuma zikiwa ndefu.

Nguo hiyo huweza kuvaliwa popote, mfano; kazini, ambapo unaweza ukavaa na sketi yenye ufupi wa wastani na itapendeza endapo itakuwa ni aina ya penseli.
Pia unaweza kuvaa shati ya aina hiyo na ‘tight’ ama kaptula fupi, ambayo mara nyingi huvaliwa maeneo ya ufukweni.

Itapendeza kama viatu vifupi, maarufu kama sandozi zitatumika.
Gauni aina ya ‘high low’ pia inaweza kuvaliwa popote,  itategemea imevaliwaje.
Endapo gauni hilo litakuwa na urefu unaostaili kuingia nayo ofisini, unaweza ukavaa hasa kwa siku kama za Ijumaa na  siyo vyema kuvaa siku ya Jumatatu.

Ikiwa gauni hilo pia litavaliwa kazini ni vizuri kama litaambatana na kiatu chenye urefu wa wastani, pamoja na pochi nzuri.

Endapo utavaa gauni hilo katika sherehe, unaweza ukavaa na kiatu kirefu, lakini kwa kuwa mara nyingi sherehe hufanyika usiku, unaweza kuvaa gauni la ‘high low’ fupi kiasi.

Wasichana wengi hupendelea vazi hilo kwa kuwa hupenda kuonyesha miguu yao na viatu walivyovivaa, hivyo aina hiyo ya mshono husaidia kuonyesha vitu kwa jinsi ulivyopendeza.

Ukivaa gauni ya aina hiyo, pia unaweza kuvaa na mkanda mwembamba ili kuweka nakshi, pia hereni na bangili, ambazo zitaendana na mtindo wa nywele uliotengeneza, ili kukufanya upendeze zaidi.

Vilevile unaweza kuvaa na kikoti kidogo, ukiwa unaenda ofisini ili kukufanya uwe mtanashati na kuonekana kiofisi zaidi.

Mbali na gauni pia kuna sketi aina ya ‘high low’ ambayo pia huweza kuvaliwa na blauzi, ambayo inaenea kwenye nguo na siyo shati kubwa ambalo huwa halipendezi.
Mara nyingi sketi ndefu hupendelewa kuvaliwa na watu wengi.

Imeandaliwa na Deborah Mgajilo