Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UREMBO ASILIA: Kabiliana na mafuta usoni kwa yai na limao

Ngozi yenye mafuta hasa usoni huwa kero kwa wanawake kwa sababu huchangia kuharibu ngozi. Chunusi ni miongoni mwa madhara yanayoambatana na ngozi yenye mafuta isipopata tiba kwa wakati mwafaka.

Maski ya mchanganyiko wa ute wa yai uliochanganywa na limao ni miongoni mwa vitu vinavyoweza kukumalizia tatizo la mafuta usoni.

Ni mchanganyiko ambao umethibitshwa kuwa sahihi ukilinganisha na maski za viwandani ambazo huchanganywa na kemikali ambazo zinaweza kuwa na madhara zaidi.

Mahitaji

-         Ute mweupe wa yai 1

-         Juisi ya limao vijiko 3

Changanya ute wa yai na juisi ya limao kisha jipake usoni na ukae na mchanganyiko huo kwa dakika 10-15. Usipake katika eneo linalozunguka macho.

Inafanyaje kazi?

Maski hii hulainisha mafuta na kuyaondoa katika ngozi na husaidia kupunguza ukubwa wa matundu katika ngozi. Asidi iliyopo katika juisi ya limao husaidia ulinganifu wa virutubisho vya ngozi.

Kwa matokeo mazuri tumia kati ya wiki 1-2 kila siku.