Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KANDA BONGO MAN: Mkali aliyeitikisa Afrika kwa mtindo wa Kwasakwasa

Kanda Bongo Man

Muktasari:

Msanii huyu kutoka Zaire ni miongoni mwa wasanii waliojitengenezea umaarufu mkubwa katika miondoko ya Soukous barani Afrika.

Kwa wafuatiliaji wa muziki wa miaka ya 80 Kanda Bongoman litakuwa si jina geni masikioni mwao.

Msanii huyu kutoka Zaire ni miongoni mwa wasanii waliojitengenezea umaarufu mkubwa katika miondoko ya Soukous barani Afrika.

Licha ya uwezo wake mkubwa katika uimbaji na utunzi umaarufu wa nyota huyu ulijengwa zaidi na muonekano wake wa kimavazi sambamba na uchezaji. Kupendelea kwake kupenda kofia za pama kulichangia kofia hizo kupachikwa jina Kanda Bongoman.

Mkali huyu alitamba na nyimbo kama Inde Monie, Iyole, Kwasakwasa, Isambe, Billi, Liza, Lela-lela, Sana, Naloti, Sai, Bed,Yonde love me na nyinginezo.

Apandapo jukwaani mashabiki wote hutegemea kufurahia burudani wa nyota huyo hasa kupitia mtindo wake maarufu wa kwasakwasa.

Sauti yake nyororo iliyobeba mashairi matata katika lugha ya kilingala na kifaransa ilimfanya Kanda Bongoman kuwa miongoni mwa watumbuizaji machachari barani Afrika.

Mzuka aliokuwa nao kwenye muziki ulimfanya nyota huyu kukacha shule ili kuingia kwenye fani hiyo ambayo aliamini ilikuwa ndani ya moyo wake.

Akiwa na umri wa miaka 18 tayari Kanda Bongoman alishaamua kuachana na masomo na kujiunga na bendi za mtaani ili kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanamuziki. Pamoja na kuwa Bongoman alifahamika zaidi mwanzoni mwa miaka ya 80 lakini sanaa ya uimbaji alianza rasmi mwaka 1973 alipojiunga na bendi ya Orchestra Belle Mambo.

Mwanamuziki Tabu Ley ndiye aliyekuwa akimvutia sana Bongoman kiasi cha kumfanya ajaribu kila njia ili siku moja na yeye awe na jina kubwa kwenye ramani ya muziki jambo ambalo lilifanikiwa.

Alidumu kwenye mbendi hiyo kwa muda wa miaka sita kabla ya kujitoa na kuanza kufanya kazi zake kama mwanamuziki wa kujitegemea.

Haikumchukua muda mrefu kwani mwaka 1981 aliweza kukamilisha albamu yake ya kwanza iliyoitwa Iyole ambayo alirekodi kwa kumshirikisha mcharaza gitaa mahiri Diblo Dibala.

Huo ndiyo ukawa mwanzo wa mwanamuziki huyu kujitengenezea umaarufu mkubwa nchini Zaire na bara zima la Afrika kwa ujumla.

Sifa zake zikaaanza kusambaa mpaka mabara mengine ambako pia alianza kupata mialiko, mwaka 1983 akapata fursa ya kutumbuiza kwenye tamasha la WOMAD nchini Uingereza.

Kuanzia hapo ikawa ni jambo la kawaida kwa Kanda Bongoman kupata mialiko ya kutumbuiza kwenye mataifa makubwa duniani ikiwemo Marekani ambako kote huko aliweza kuusambaza mtindo wake wa kwasakwasa.