KWA TAARIFA YAKO: Jennifer Lopez anaogopa panya hata katika runinga
Pamoja na kuwa na miaka zaidi ya 50 mwimbaji Jennifer Lopez amesema kuwa anaogopa sana panya.
Akihojiwa katika kipindi cha Burning Question kinachoe ndeshwa na Ellen, alisema hajawahi kuishi eneo lenye panya, lakini anawaogopa sana hata akiwamo katika filamu.
“Najua wana akili, Ila ni wasumbufu sana, sipendi panya,” alisema Lopez.
Lopez au J.Lo, pia aliitaja tabia mbaya ambayo ameshindwa kuiacha katika maisha yake kuwa ni kuchelewa, hususani anapolala ni mvivu kuamka.
“Siku za mwanzo nikiwa naanza uigizaji filamu nilipata wakati mgumu kuwahi eneo la kupigia picha, kwa sababu nina tabia mbaya ya kuchelewa kuamka . “Hii huanzia usingizini, nikilala nakuwa mvivu kutoka kitandani hata kama nikiwa macho yaani sina usingizi kazi inakuwa kuamua sasa natoka kitandani, napambana kuiacha tabia hii,” alisema Lopez huku akicheka.