Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal, PSG zampigania Gibbs-White

Kiungo mshambuliaji wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White. Picha na Maktaba

Muktasari:

  • Muingereza huyo anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji lakini pia anaweza kutumika vizuri katika nafasi ya winga.

Nottingham, England. Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2025/2026 imejirudia tena lakini safari hii ni katika vita ya usajili.

PSG iliyochukua ubingwa na Arsenal iliyoshika nafasi ya pili zote zimeingia vitani kuwania saini ya mshambuliaji wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White.

Kiwango bora ambacho kiungo mshambuliaji huyo amekionyesha katika msimu uliomalizika kimeonekana kuzikosha timu hizo ambazo kila moja imemuweka katika orodha ya wachezaji inaowahitaji.

Kwa Arsenal, Gibbs-White (26) anaonekana kama mtu sahihi wa kuongeza ufanisi wa kutengeneza nafasi za mabao na kufunga kutokana na uwezo wa mchezaji huyo kucheza kwa ufasaha katika nafasi tofauti uwanjani.

Muingereza huyo anamudu kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji lakini pia anaweza kutumika vizuri katika nafasi ya winga.

Kwa upande wa PSG, Morgan Gibbs-White anatazamwa kama mbadala sahihi wa

Khvicha Kvaratskhelia ambaye ripoti zinadai kwamba ni miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi kipaumbele cha kwanza katika usajili.

Msimu uliomalizika, mchezaji huyo alifunga idadi ya mabao 18 katika mechi za mashindano yote aliyoichezea Nottingham Forest kubaki katika Ligi Kuu England.

Pamoja na kiwango hicho bora ambacho Gibbs-White amekionyesha, hakupata fursa ya kuwa miongoni mwa wachezaji 26 wa timu ya Taifa ya England ambao watashiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026.

Mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa nyota waliowania tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya England katika msimu uliopita ambayo iliangukia kwa Bruno Fernandes wa Manchester United.

Pia alikuwemo katika kundi lililowania tuzo ya Mchezaji Bora England ya BBC ambayo mshindi alikuwa ni Declan Rice wa Arsenal.

Gibbs-White pia jina lake limejitokeza katika ushindani wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England inayotolewa na Chama cha Wanasoka wa Kulipwa England (PFA).