Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Euro 2024 rekodi na zote 16 hizi hapa

Munich, Ujerumani. Michuano ya Euro 2024 hatua ya makundi imefikia tamati jana Jumatano ambapo sasa timu 16 zimetambulika zitakazoenda kucheza hatua inayofuata kuwania taji linaloshikiliwa na Italia.

Michuano hiyo iliyoanza kuunguruma Juni 14, mwaka huu huko nchini Ujerumani, ilianza kwa kuzishirikisha timu 24 zikipangwa kwenye makundi sita na kuchezwa katika majiji 10.

Timu mbili za juu kutoka kila kundi zimefuzu moja kwa moja kucheza hatua ya 16 bora, huku nne zilizomaliza nafasi ya tatu na kuwa na matokeo mazuri zikiungana nazo.

Kabla ya jana, zilikuwa zimechezwa jumla ya mechi 32 na kufungwa mabao 74 kukiwa na wastani wa mabao 2.31 kwa mechi. Wanaoongoza kwa mabao ni Georges Mikautadze (Georgia) mwenye mabao matatu, Niclas Füllkrug (Ujerumani), Jamal Musiala (Ujerumani), Cody Gakpo (Uholanzi), Ivan Schranz (Slovakia) ambao kila mmoja ana mabao mawili.

Katika hatua ya makundi, rekodi kadhaa zimewekwa kwa timu na mchezaji mmojammoja, hapa kuna baadhi yake.


02

Ufaransa imefunga mabao mawili katika Kundi D baada ya kucheza mechi tatu ikiwa ni idadi ndogo ya mabao kwenye michuano ya Ulaya hatua hiyo. Ilishuhudiwa mara mbili ikifanya hivyo mwaka 1992 na 2008 ambapo iliishia hatua ya kwanza tu. Pia England nayo imefunga mabao mawili hatua hiyo ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu mwaka 1992.


535

Kylian Mbappe amefunga bao lake la kwanza katika michuano hiyo ya Ulaya baada ya kucheza kwa dakika 535. Sasa amefikisha mabao 13 katika timu ya taifa akimfikia mkongwe Just Fontaine.


01

Kitendo cha Donyell Malen kujifunga katika mchezo dhidi ya Austria, imekuwa ni mara ya kwanza kwa kikosi cha Uholanzi kuruhusu bao la kujifunga kwenye michuano ya Euro huku likiwa ni la saba kwa mwaka huu ndani ya Euro 2024.


04

Katika mechi nne za mwisho ambazo Austria imeongoza kwa kufunga bao kwenye michuano ya Euro, imeshinda zote, huku ikifanikiwa kuzuia kichapo cha nane kutoka kwa Uholanzi walipokutana kwenye michuano yote tangu mwaka 1984 baada ya juzi kushinda 3-2.


133

Nyota wa Denmark, Christian Eriksen amefanikiwa kucheza mechi 133 akiwa na kikosi hicho akivunja rekodi ya Simon Kjaer kwa kucheza mechi nyingi katika timu ya wanaume ya nchi hiyo.


07

Idadi hiyo ya mabao iliyofungwa katika Kundi C mwaka huu inalingana na ile ya mwaka 2016 kutoka Kundi kama hilo (Ujerumani 3, Northern Ireland 2, Poland 2 na Ukraine 0) ikiwa ni mabao machache zaidi kufungwa katika kundi moja la Euro tangu 1980.


Timu zilizofuzu 16 bora

Ujerumani
Uswisi
Hispania
Italia
England
Denmark
Slovenia
Austria
Ufaransa
Uholanzi
Ureno
Uturuki
Georgia
Slovakia
Ubelgiji
Romania