Gomes atoa sababu za kuwaacha akina Morrison

Friday March 05 2021
simbapic
By Thobias Sebastian

Khartoum. Kocha wa Simba, Didier Gomes amewacha wachezaji watano Dar es Salaam kutokana na sababu mbalimbali ambao ni, vizuri Bernard Morrison, Ibrahim Ame, Junior Lokosa, Said Ndemla na Parfect Chikwende.

Gomes alisema kila mchezaji amebaki kutokana na sababu mbalimbali lakini kubwa aliokwenda nao Sudan ndiyo alikuwa na mahitaji nao na mechi yenyewe.

"Nilikuwa nahitaji wachezaji wasipungue 25 katika safari hii na nimefanikiwa kuja nao hapa Sudan wengine waliobaki Tanzania nitawajumuisha katika safari nyingine.

"Kubaki kwao kuna sababu mbalimbali ambazo zipo nje ya uwezo wao mpaka wakashindwa kusafiri ila hawa ambao wapo huku watawawakilisha vizuri.

"Kila mchezaji, ambaye tumesafiri nae hapa Khartoum Sudan yupo fiti na anaweza kucheza jukumu limebaki kwangu kuona namna gani, ambavyo naweza kuchagua 11, ambao wataanza na saba ambao watakuwa benchi," alisema Gomes.

Wachezaji hao waliobaki Dar es Salaam, wanatakiwa kuwa na programu maalumu ya kufanya mazoezi akiwemo Morrison ambaye alishindwa kufanya mazoezi na wenzako tangu mechi na Al Ahly alipomalizika kutokana na kuumwa.

Advertisement

Wachezaji hao wanatakiwa kufanya mazoezi ili kuweka miili yao sawa na wenzao watakapo rejea utimamu wa kike ili usiwe umepotea.

Advertisement